Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nabi atoa kauli nzito

MASHABIKI wa Yanga wamekuwa wanyonge wakiona watani wao wakifurahia wao kudondosha pointi mbili lakini kocha wao Nasreddine Nabi amekutana na wachezaji wake na kuwaambia; “Tulieni ntalibeba mwenyewe”

Nabi ameliambia Mwanaspoti kuwa amewaambia wachezaji wote kwamba hataki kuona wanakuwa wanyonge kwani anayepaswa kulaumiwa kwa matokeo ya suluhu ya juzi ni yeye. “Natakiwa kulaumiwa mimi natangulia mbele kwa niaba yao nimewaambia sitaki kuona wanainama vichwa chini kila mmoja ainue kichwa na tuendelee na mapambano,” alisema Nabi.

“Vijana wangu wamecheza vizuri walifanya kila ambalo walitakiwa kulifanya lakini kuna wakati tunatakiwa kujiandaa na matokeo ya namna hii tunatakiwa kurudisha akili zetu katika mapambano na sio kuanza kuhuzunika sana,” aliongeza Kocha huyo.

“Tulitakiwa kubadilika kutumia njia za pembeni kutafuta ushindi lakini mambo hayakuwa hivyo hatukuwa na ubora na hili limetokana na watu wazuri wa kutumia njia hiyo baadhi ni wagonjwa.

“Angalia juzi tulilazimika kumtumia Job (Dickson) kama beki wa pembeni lakini tunarudi katika maandalizi yetu na naamini tutakuwa bora zaidi katika mchezo ujao.”


SENZO AKAZIA

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mazingisa ameliambia Mwanaspoti kwamba; “Ligi ni mbio ndefu hakuna ambaye atakuwa na uhakika wa kushinda kila siku kitu bora tunachotakiwa kukifanya ni kujiandaa kwa ubora kwa asilimia mia moja,tusitarajie wepesi sikuzote, matokeo tuliyopata kipimo sahihi.”