Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nabi apewa saa 48 Kaizer Chiefs

ALIYEKUWA kocha wa Yanga,  Nasreddine Nabi amesema ndani ya saa 48 mustakabali wake na  Kaizer Chiefs utakuwa umejulikana.

Nabi aliachana na Yanga baada ya kumalizika kwa msimu uliopita akiwa ameipa timu hiyo Ubingwa wa Ligi Kuu Bara, Kombe la FA na Ngao ya Jamii, lakini akiwa ameifikisha fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kaizer Chiefs imekuwa ikitajwa muda mrefu kuwa inamhitaji kocha huyo, jana akihojiwa na gazeti maarufu la Afrika Kusini, The South Afrika alisema mazungumzo yanaendelea na ndani ya saa 48 watakuwa wameshamalizana.

“Kwa sasa ni ngumu kukupa taarifa, kwanza tunakuheshimu wewe na chombo chako cha habari, lakini tambua kuwa tunaendelea kuzungumza na viongozi wa Chiefs kupitia wakala wangu na ndani ya saa 48 tutakuwa tumeshakamilisha na kufahamu nini kinaendelea.”

Alipoulizwa kuhusu kambi ya Kaizer Chiefs, kocha huyo mwenye uzoefu mkubwa wa soka la Afrika, alisema hawawezi kutoa taarifa zaidi ya hiyo iliyopo bali usubiriwe muda sahihi.