Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mzuka wa Kisinda wamuibua Mukoko

YANGA wanajipika kivyao kule katika kambi yao ya Avic na fahamu kwamba kuna ulinzi mkubwa umeimarishwa kila kona ya ukuta wa kambi hiyo lakini habari njema ikawa kurejea kwa staa wao mwenye kasi pengine kuliko yeyote katika Ligi Kuu Bara na sasa kiungo mmoja akafungua mdomo wake akisema ushindi kwao upo.

Winga aliyerejea ni Tuisila Kisinda ambaye amepona maumivu ya mkono wake na jana juzi alionekana kubeba vyuma vizito huku jana akirejea uwanjani.

Simba ina kikosi kipana, lakini kurejea kwa Kisinda sio taarifa njema kwa Wekundu hao kuelekea mchezo wao wa Mei 8 pale Uwanja wa Mkapa ambapo Wanamsimbazi wanamkumbuka winga huyo Mcongo alivyowakimbiza mabeki wao akiwamo Joash Onyango katika derby iliyopita uwanjani hapo hadi kusababisha penalti iliyopa Yanga bao la kuongoza kabla ya Onyango mwenyewe kusawazisha na ngoma kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Akizungumza na Mwanaspoti, kiungo mkabaji wa Yanga, Mukoko Tonombe alisema mzuka wao wa kwanza katika kikosi chao ni kurejea kwa Kisinda akiwa ndio staa pekee aliyekuwa shakani kucheza derby hiyo.

Mukoko alisema Kisinda anarudisha nguvu katika safu yao ya ushambuliaji ambayo ilitetereka baada ya kumkosa katika mechi mbili zilizopita.

“Kisinda ni mchezaji muhimu anajua kucheza mechi kubwa kama hizi, kama uliona, kuna kitu kilipungua kule mbele katika mechi mbili zilizopita, unajua tunakwenda kwenye mechi kubwa ni muhimu tukawa kamili,” alisema Mukoko ambaye usajili wake ulimuhusisha winga huyo wakitua sambamba wakitokea klabu moja ya AS Vita.

“Hii ni habari njema kwa yeyote anayependa Yanga, lakini pia hata kwa makocha ambao sasa watakuwa na upana wa machaguo ya wachezaji kuelekea mchezo huo, kasi ya Kisinda ni kitu ambacho hata Simba wanajua ni hatari kwao.”

Akizungumzia mchezo huo kwa ujumla, Mukoko alisema wanakwenda kukutana na timu kubwa yenye wachezaji wazuri na kwamba mchezo huo utaamuliwa na wachezaji bora.

“Hii ni mechi ya pili kwangu dhidi ya Simba hapa kwenye ligi. Ni mechi kubwa, lazima tutambue kwamba Simba ni timu kubwa, ina wachezaji bora. Ila hii ni mechi ya derby na itaamuliwa na wachezaji wakubwa wanaojua kuhimili presha.

“Yanga tuko sawa katika eneo hili, sidhani kama itakuwa ni Yanga ile iliyocheza mechi chache zilizopita. Kuna hamasa kubwa ndani ya timu hivi sasa.”

Aidha, Mukoko ambaye ni nahodha wa tatu katika kikosi hicho, alisema uwepo wa kocha wao Nesreddine Nabi ni kitu kingine bora ambapo licha ya upya wake katika soka la Tanzania lakini anaijua Simba.