Mwamnyeto aishtukia Belouizdad mapema

Muktasari:

  • Yanga itakuwa wageni wa Belouizdad katika mechi ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ijumaa hii na Mwamnye-to, aliliambia Mwanaspoti ugumu wa ratiba unawafanya wachezaji waliopo Stars kucheza kwa maelekezo na akili zaidi wakitambua umuhimu wa nafasi zao Stars na Yanga.

NAHODHA wa Yanga, Bakari Mwamnyeto aliyekuwa sehemu ya kikosi cha Taifa Stars kilichopata ushindi wa bao 1-0 mbele ya Niger kwenye mechi za kuwania Fainali za Kombe la Dunia 20246, amesema wanakiwasha Stars, huku wakijua wana kibarua kigumu kwa CR Belouizdad ya Algeria.

Yanga itakuwa wageni wa Belouizdad katika mechi ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ijumaa hii na Mwamnye-to, aliliambia Mwanaspoti ugumu wa ratiba unawafanya wachezaji waliopo Stars kucheza kwa maelekezo na akili zaidi wakitambua umuhimu wa nafasi zao Stars na Yanga.

“Unajua ukuta wa Yanga ndio ukuta wa Stars tupo hapa kuipambania nchi na bado tutahitajika kwenda kuen-delea tulipoishia kwa kuhakikisha timu inaanza vyema mchezo wake wa kwanza kwenye kundi D,” alisema Mwamnyeto ambaye yeye, Dickson Job na Ibrahim Bacca wanatumika kotekote wakiwa pamoja.

“Kocha Miguel Gamondi kaniambia mimi nikiwa kama nahodha natakiwa kuwaongoza wenzangu ninaocheza nao pamoja Dickson Job, Mudathir Yahya, Ibrahim Abdallah ‘Bacca’ kuhakikisha tunakuwa makini zaidi tusipate shida, Yanga na Stars zinatutegemea,” aliongeza nahodha huyo.

Mwamnyeto alisema hawatakuwa na muda wa kupumzika kwani wakimalizana na Morocco mechi itaka-yopigwa kesho,  wataunga moja kwa moja uwanja wa ndege tayari kwa ajili ya kwenda kuungana na Yanga kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya CR Belouizdad.