Prime
MVP azitosa Yanga, Simba, sababu yatajwa
WAKATI Yanga, Simba na Singida Black Stars zikionyesha nia ya kumuhitaji mchezaji bora wa Ligi ya Kenya (MVP) msimu huu, Mghana Enock Morrison aliyekuwa anacheza Gor Mahia FC dili hiyo imeingiliwa kati wa Wasudani.
Awali Singida ilionyesha nia ya kuhitaji saini ya nyota huyo tangu dirisha dogo la Januari 2026, ingawa baada ya kiwango bora alichokionyesha akiwa na Gor Mahia, kilianza kuzivutia klabu nne za Tanzania kwa ajili ya msimu ujao.
Miongoni mwa timu zilizoonyesha nia ya kumuhitaji mbali na Yanga, Simba na Singida, nyingine ni TRA United ambazo hata hivyo zimeishindwa vita hiyo, baada ya mabwenyewe wa Al Merrikh SC ya Sudan kukamilisha dili hilo mapema iwezekanavyo.
Taarifa kutoka Sudan zinaeleza uongozi wa timu hiyo ulifanya mazungumzo ya moja kwa moja na kam-bi ya mchezaji huyo na kufikia muafaka wa kujiunga na kikosi hicho, baada ya miamba wengine kuo-nyesha nia bila ya kufanya makubaliano yoyote.
Licha ya kushinda mchezaji bora wa msimu yaani (MVP), ila Enock alishinda pia Tuzo ya kiungo bora wa msimu wa Ligi Kuu ya Kenya, huku akiisaidia Gor Mahia kutwaa ubingwa, baada ya kufikisha pointi 69, nyuma ya AFC Leopards iliyokuwa na 64.
Katika Ligi Kuu ya Kenya msimu huu, nyota huyo alichangia mabao saba ya Gor Mahia FC baada ya kufunga matatu na kuasisti manne, huku akiibuka pia kidedea kwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mechi, baada ya kufanya hivyo, mara 15.
Nyota huyo aliyezaliwa Januari 18, 2000, akiwa na uwezo wa kucheza kiungo wa kati kwa ufasaha mkubwa, huku akitokea pia upande wa kulia na kushoto, amezichezea timu mbalimbali, zikiwemo za King Faisal FC na Asante Kotoko zote za kwao Ghana.