Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Muacheni Sanchez aishi maisha anayoishi

NIKIWA nimejituliza zangu kwenye kochi kuu kuu, huku mkononi nimeshikilia kitabu cha The Spy Who Loved Castro, kilichoandikwa na mwandishi pekee wa kike niliyewahi kuelewa thamani ya vidole vyake mwanamama Mjerumani,  Marita Lorenz,  ghafla fikra fikirishi zikanitawala kichwani mwangu.
Sura ya kitoto cha mtaani, chokoraa aliyefanya kila aina kazi chafu ikanijia, jina lake likanitawala kwenye ubongo wangu, akili ikanambia kuwa, kwasasa hana chakupoteza kwenye maisha yake, amepata kile alichowahi kukiwaza.
Huyu ni Alexis Sanchez, mchezaji mwenye historia ya kutisha na kusikitisha kwa wale waliobahatika kuisoma, kwenye maisha yake tokea alipokuwa kijana mdogo msamiati uliokuwa unasambaa kwenye mirija ya ubongo wake ni pesa tu, ndio maana hakuona tabu hata kuosha magari, kusafisha vyoo ili mkono wake uende kinywani.
Ndoto ya mpira ilimjia wakati anacheza mpira, kwake ukimuuliza kati ya mpira na pesa bora nini, atachagua pesa tu, ndio maana hata wakati alipokuwa anatajwa kuondoka Arsenal kulikuwa na lundo la klabu zinazohitaji saini yake, lakini yeye aliangalia wapi kuna mpunga mkubwa.
Kwake namba za akaunti yake ya benki ni bora kuliko hata namba ya idadi ya vikombe vya uwanjani. Mapenzi yake na meseji za miamala ya kifedha huwa yanazidi maradufu pale taswira ya kuungua na Jua katikati ya Jiji Tocopilla, huku watu wakiwa wamemzunguka wakati anaonesha mchezo wa Sarakasi.
Hasira humpanda zaidi pale anapovuta taswira ya namna mama yake alivyonyeshewa na mvua, ili kuwatafutia chakula baada ya Baba yao kuwatelekeza.
Muacheni huyu Sanchez aishi maisha anayoishi hivi sasa, wala msishangae kwanini kiwango chake ni kibovu, maana yeye wala hajali kabisa kuhusu hilo, alichotaka kutimiza ametimiza tayari na hakuna deni analodaiwa.
Ukifika pale Mji Mkuu wa nchi ya Chile, Santiago, jina pekee wanalomwita wao ni Shujaa, mabango yaliyochorwa kwa jina lake utayapata kila kona mwa jiji hilo, huku ukitia mguu pale kwenye Kimji kidogo cha Tocopilla , maarufu kwa kuishi watu maskini, kila utakayemuuliza kuhusu Sanchez atakwambia kwamba huyo ni Mfalme wao.
Wanaamini kuwa hana deni kwa upande wao, kitendo cha kuisaidia timu hiyo kuchukua Ubingwa wa Copa America mara mbili na zile penati zake za mwisho kwenye michezo ya Fainali, kinawafanya watu wa Chile waamini kuwa Sanchez ana haki ya kufa hata leo na hawamdai tena.
Hakuna la kupinga juu ya kipaji alichobarikiwa, ni mmoja ya wachezaji wenye vipaji vilivyotukuka kupita maelezo, na ndio maana akafika hapo alipofikia, lakini hata siku moja hajawahi kukiweka kipaji chake juu ya pesa, siku zote pesa kwake huwa zinakaa juu ya kipaji, akiamini kama atakipa nafasi kipaji kutawala anaweza akarudia tena zile zama za kupiga deki vyooni ili akamnunulie Mama yake Panaldo.
Muacheni Sanchez aishi maisha haya anayoshi, msimbeze kwa kiwango chake cha sasa hakuna anajidai amefanya kile alichotamani kufanya wakati akiwa hana uwezo huo. Angeachaje pauni 500,000 kwa wiki kutoka United, ili akachukue taji na Manchester City? Mwacheni jamani alipotoka ni shimoni na hahitaji kurudi tena huko.