Mtwara wanataka timu mbili ligi kuu
Muktasari:
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara, Yusuph Nanilla alipokuwa anajibu swali aliloulizwa na mwandishi wa habari hizi juu ya hatma ya timu ya Ndanda FC inayo wawakilisha Wanakuchele kwenye ligi kuu na ipo katika hatari ya kushuka.
Mtwara: Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara, kimesema kina mikakati ya kuhakikisha wanakuwa na timu za soka zaidi ya moja, kwani wao ndio wanashikilia uchumi mkubwa wa Tanzania.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara, Yusuph Nanilla alipokuwa anajibu swali aliloulizwa na mwandishi wa habari hizi juu ya hatma ya timu ya Ndanda FC inayo wawakilisha Wanakuchele kwenye ligi kuu na ipo katika hatari ya kushuka.
“Tumemwagiza mkuu wa mkoa kama serikali kwa sababu ni ilani yetu na moja kati ya vitu vinavyotugusa na vimetuumiza. Wiki ijayo nitapata lolote kuhusu suala la Ndanda,”amesema Nanilla
“Mikakati ambayo tunaiunda sio lazima Mtwara iwe na timu moja, kuna mikoa ina timu mpaka tatu, kwa nini Mtwara ambao tunashikilia uchumi mkubwa Tanzania tuwe na timu moja ya Ndanda na kwa nini Ndanda inafikia hatua ile?" alihoji Nanilla.
Lakini, wakati anasema wana mikakati, tayari timu hiyo ipo katika hatari ya kushuka, imebakiza mechi mbili ambazo zitapigwa katika Uwanja wa Nangwanda, Sijaona.