Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtanzania kuanza na mwenyeji ndondi za dunia

Muktasari:

  • Ratiba ya mashindano ya 13 ya IBA ya ubingwa wa dunia yatafunguliwa kesho Alhamisi mjini  New Delhi, Tanzania ikiwakilishwa na mabondia wawili.

Beatrice Nyambega atafungua dimba kwa mabondia wa Tanzania keshokutwa Ijumaa kwenye mashindano ya ngumi ya dunia kwa wanawake yatakayofunguliwa kesho nchini India.

Beatrice atacheza na mwenyeji, Jasmine Jaismine kwenye uzani wa light kilogramu 60 kuanzia  saa 9.30 alasiri ya Tanzania akiwa kona ya bluu.

Mtanzania mwingine, Rahma Maganga atapanda ulingoni Jumamosi dhidi ya Mkenya,
Kwenye uzani wa Minimum kilogramu 48.

 Rahma atacheza na Christine Ongare bondia aliyewahi kuzichapa naye Januari mwaka huu kwenye mashindano ya klabu bingwa Afrika Mashariki.

Mtanzania  huyo alichapwa kwa pointi za majaji  3-2 na kwenye mashindano ya dunia anasema amedhamiria kulipa kisasi.