Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtanzania asajiliwa Brentford

BRENTFORD Pict

Muktasari:

  • Kiungo chipukizi mwenye asili ya Tanzania, Andrew Noni, amesajiliwa katika akademi ya Brentford United ya England, hatua inayomuweka karibu zaidi na ndoto ya kucheza Ligi Kuu England.

TANZANIA imeendelea kuwa moja ya nchi zinazotajwa kuwa na vipaji vikubwa vya soka baada ya nyota wake kusajiliwa timu mbalimbali za Ulaya.

Kiungo chipukizi mwenye asili ya Tanzania, Andrew Noni, amesajiliwa katika akademi ya Brentford United ya England, hatua inayomuweka karibu zaidi na ndoto ya kucheza Ligi Kuu England.

Brentford imempa mkataba wa miaka miwili katika mfumo wake wa maendeleo ya vijana, ikionyesha imani kubwa kwa uwezo wake.

BREN 01

Noni, mwenye umri wa miaka 15, anacheza nafasi ya kiungo wa kati anayeanzisha mashambulizi lakini pia ana uwezo wa kucheza kama kiungo mkabaji. Ana urefu wa takribani futi sita, jambo linalomsaidia kutawala mipira ya juu na kuonyesha uimara katikati ya uwanja.

Taarifa zilizotolewa hadi sasa zinaonyesha Brentford ndiyo klabu ya kwanza kubwa kumchukua rasmi katika mfumo wake wa akademi, huku kukiwa hakuna rekodi za kuchezea akademi nyingine kabla ya usajili huo.

Noni ni Mzimbabwe mwenye asili ya Tanzania, anaongeza idadi ya vijana wanaochipukia na kusajiliwa kwenye akademi kubwa duniani.

BREN 02

Brentford ni moja ya akademi zilizojitengenezea sifa ya kuibua na kukuza vipaji vya vijana kabla ya kuwapa nafasi ya kucheza katika timu za wakubwa.

Hivyo, Noni anaingia katika mazingira yatakayompa nafasi ya kuendelea kujifunza, kuimarika kiufundi na kimwili, huku akipigania nafasi ya kupanda hatua kwa hatua kuelekea timu za wakubwa.