Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtambo wa mabao warejesha mzuka Geita

BAADA ya kurejea kutoka Sweden kwenye majaribio, mshambuliaji wa Geita Gold, Valentino Mashaka aliibeba timu yake kwa kuifungia bao muhimu katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji.

Ushindi huo ulikuwa wa kwanza kwa Geita Gold katika mwaka huu 2024 kwani mara ya mwisho kupata pointi tatu kabla ya mchezo huo ilikuwa Desemba 21 waliposhinda dhidi ya Singida FG.

Hata hivyo, katika ushindi huo, Mashaka ndiye aliifungia bao Geita Gold ambapo tangu aondoke nchini kwa kujaribu bahati huko Sweden timu hiyo ilikuwa haijapata ushindi wowote.

Timu hiyo ya mjini Geita ilicheza mechi sita mfululizo ikipoteza mitatu dhidi ya Simba 1-0, Azam 2-1, Ihefu 3-1, sare dhidi ya KMC, Mashujaa na Kagera Sugar ikiwa imefungwa mabao tisa na kufunga manne.

Mashaka ambaye anaongoza kwa mabao klabuni hapo akiwa amefunga matano katika Ligi Kuu ametwaa tuzo mbili za Mchezaji Bora wa Desemba na Oktoba kwa timu hiyo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mashaka alisema anashukuru kurejea na kiwango chake akieleza kuwa nia yake ni kuisaidia timu kuondokana na matokeo yasiyoridhisha waliyonayo kwa sasa.

“Nashukuru Mungu nimeendelea kuwa mchezaji muhimu kwa timu yangu na kuisaidia kupata ushindi, siri kubwa ni kujituma, kufuata maelekezo na kuendelea kupambana,” alisema nyota huyo.

Afisa Habari wa timu hiyo, Samwel Dida, alisema dili la nyota huyo kwenda Sweden lilifanywa kimya kimya ili kuondoa wasiwasi kwa mashabiki na kwamba iwapo atafaulu ataondoka msimu ujao.