Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msanii Radio afariki dunia

Uganda. Msanii wa muziki wa nchini Uganda, Moses Ssekibogo maarufu Radio amefariki dunia leo Alhamisi saa sita usiku.

Mwandaaji wa matamasha, Balaam Barugahara alimthibitishia mwandishi wa Dailly Monitor kuwa msanii huyo alifariki wakati akiendelea na matibabu hospitalini.

Msanii huyo ambaye alikuwa akifanya vizuri na mwenzie Weasel,  tangu Januari 23 mwaka huu hali yake ilikuwa mbaya kutokana na majereha aliyoyapata kwenye ugomvi klabu ya De Bar kisha kupelekewa jijini Entbebbe kwa matibabu zaidi.

Rais wa Uganda, Yoweri Museven alitoa Sh30 milioni jana Jumatano kwa ajili ya  matibabu ya msanii huyo.

 Pia kulikuwa na maombi maalumu yalikuwa yameandaliwa kwa ajili ya kumuombea ambayo yalitarajiwa kufanyika Februari 4 mwaka huu katika Kanisa la Light the World.