Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mrisho Ngassa atoa angalizo Simba

Muktasari:

  • Mohammed IV nchini Morocco huku winga wa zamani wa Yanga, Mrisho Ngassa akiwataka kuwa makini zaidi na waarabu hao.

LEO Ijumaa kuanza saa 4:00 usiku, Simba itakuwa uwanjani kucheza mechi ya marudiano ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca kwenye Uwanja wa

Mohammed IV nchini Morocco huku winga wa zamani wa Yanga, Mrisho Ngassa akiwataka kuwa makini zaidi na waarabu hao.

Mbali na kuzungumzia mchezo huo pia amewaonya Yanga kutobwetekeza kwenye mechi yao ya marudiano hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rivers United ya Nigeria, mechi itakayochezwa Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ngassa alisema timu zote zina nafasi ya kufuzu hatua ya nusu fainali kwenye michuano hiyo ya Caf lakini upande wa Simba watakutana na ugumu kidogo kutokana na namna waarabu hao wanavyocheza wanapokuwa nyumbani.

"Mpira ni dakika 90 lakini ndani ya hizo dakika unatakiwa kuangalia na kuongeza umakini zaidi juu ya mpinzani wako, Yanga wamecheza na timu ambayo inaonekana kama ina tatizo kidogo lakini hiyo isiwe kigezo cha kuuchukulia mchezo huo kama wa kawaida kwao, wanaweza kuja kivingine, wapambane kama ni mechi ya kwanza.

"Simba wanaenda kukutana na timu ambayo inajua kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani, waarabu kwao hawakubali kufungwa kirahisi, ila naamini kama watakuwa makini na mbinu zao watashinda na kusonga mbele," alisema Ngassa aliyewahi kuichezea timu kama Taifa Stars, Azam FC, Simba na Free State ya Afrika Kusini

Katika mechi zao za awali Simba ilishinda bao 1-0 bao lao lilifungwa na Jean Baleke wakati Yanga wao wakishinda ugenini mabao 2-0, mabao yote yakifungwa na Fiston Mayele.