Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mpole ashtuka, aanza kujifua mapema

MPOLE Pict

Muktasari:

  • Mfungaji Bora huyo wa Ligi Kuu msimu wa 2021-2022, amesema licha ya kukaa nje tangu Januari, hakuna kilichoharibika kutokana na menejimenti imara inayomsimamia kwa kila kitu ikiwamo kuwa na programu za mazoezi kwa muda wote.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Geita Gold, FC Lupopo ya DR Congo na Pamba Jiji, George Mpole, aliye nje ya uwanja tangu dirisha dogo la usajili lilipofungwa Januari mwaka huu, ameshtuka na kuanza kujifua mapema akijiandaa kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Mfungaji Bora huyo wa Ligi Kuu msimu wa 2021-2022, amesema licha ya kukaa nje tangu Januari, hakuna kilichoharibika kutokana na menejimenti imara inayomsimamia kwa kila kitu ikiwamo kuwa na programu za mazoezi kwa muda wote.

Msimu huu Mpole aliichezea Pamba Jiji aliyojiunga nayo akitokea FC Lupopo, lakini aliamua kuachana nayo kwa taratibu zinazokubalika kwa pande zote katika dirisha dogo akiwa ameifungia mabao mawili.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mpole alisema mkataba aliosaini na menejimenti yake una vipengele vya kumtafutia timu na kumsimamia programu ya mazoezi anapokuwa nje ya kazi.

“Menejimenti inayonisimamia ni ya watu wanne kutoka nje, ndio inayosimamia programu yangu ya mazoezi kuhakikisha nakuwa fiti, ndio maana sijapata changamoto yoyote ya kunisumbua, kuhusu kulipana inatokana na wao wanapopata timu wanachukua chao nabakia na changu,” alisema Mpole na kuongeza;

“Uongozi wangu upo katika mazungumzo na timu za nje, siwezi kuzitaja ila kila kitu kinakwenda sawa, hivyo msimu ujao lolote linaweza likatokea.”

Mbali na hilo alisema kukaa nje ya kazi kumemsaidia kusimamia vitu vyake, ambavyo anatarajia kuvifanya baada ya maisha ya mpira wa miguu.

“Nina shughuli zangu nje ya soka, nikitoka katika mazoezi nakwenda kuzisimamia, nimejifunza kitu kikubwa sana, hivyo najua niboreshe wapi, jambo jingine la msingi kabisa mimi ni mtu ninayekubali kuzipokea nyakati zote kisha nasonga mbele ndiyo maana sina mawazo yanayonisumbua,” alisema Mpole aliyewahi pia kuitumikia kwa vipindi tofauti timu ya taifa, Taifa Stars.