Prime
Mosimane: Nabi apewe timu, ila...
Kocha mpya wa Al Wahda ya Falme za Kiarabu (UAE), Pitso Mosimane amesema Nasreddine Nabi ana vigezo vyote kuwa kocha wa Kaizer Chiefs.
Mosimane ameyasema hayo akiwa nchini Afrika Kusini alipoenda kwenye mapumziko baada ya kusaini timu yake mpya pia kuzindua shule yake ya soka.
Alipoulizwa kwenye mahojiano kuhusu Nabi anafaa kuinoa Kaizer alisema; "Ni mtu mzuri na kocha mzuri pia, ameshinda makombe matatu mara mbili mfululizo, mimi nimefanya hivyo ila kwa miaka tofauti,"
Mosimane amempa angalizo Nabi kuwa soka la Afrika Kusini ni tofauti na Tanzania ambalo timu kubwa zinaangaliwa zaidi ambazo ni Simba, Yanga na Azam.
"Anajua stresi na presha ya kuleta matokeo. Najua atahimili vyote na amethibitisha hilo kwa kuipeleka Yanga fainali Kombe la Shirikisho," ameongeza Mosimane
Kuhusu suala la kuchukua benchi la ufundi ambalo Nabi aliwapa sharti hilo Kaizer, Mosimane amesema ni muhimu kwa levo waliyofikia kwenda sehemu mpya na benchi lako la ufundi.