Mo: Uwezo wa kushinda leo tunao

Tuesday February 23 2021
mo pic
By Thobias Sebastian

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohammed Dwji ‘Mo’ amewatia moyo wachezaji wa timu hiyo akisema kila kitu kinawezekana na kuwataka nyota hao kusaka pointi tatu mbele ya Al Ahly leo.

Akizungumza juzi wakati wa mazoezi ya mwisho ya kikosi cha Simba, Mo alisema kila kitu kinawezekana katika soka, huku akiwa na imani kubwa kuwa Simba itarudia kiwango zaidi ya kilichoonyeshwa wakati wakiilaza miamba hiyo kwa bao 1-0. Simba iliichapa Al Ahly katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Mkapa kwa bao 1-0, ushindi uliochangia kuivusha timu hiyo katika hatua ya mtoano kabla ya kutolewa na TP Mazembe, mwaka juzi.

Advertisement