Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkude aishtaki METL, ataka fidia Sh1 bilioni

Mchezaji wa Klabu ya Yanga, Jonas Mkude amefungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akiidai Kampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited (METL) fidia ya Sh 1 bilioni kwa kutumia picha zake katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Instagram na Twitter bila idhini yake.

Mkude amefungua kesi ya madai 192 ya mwaka 2023 mbele ya Jaji Butamo Philip dhidi ya kampuni hiyo akiidai fidia hiyo Kwa kuvunja haki yake ya msingi.

Mkude amejiunga na Yanga msimu huu akitokea Simba aliyotumikia kwa misimu 12.