Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Minziro kukwepa mtego wa play-off

MINZIRO Pict

Muktasari:

  • Tayari Kagera Sugar na KenGold zilizopo nafasi ya 16 na 15 mtawalia zimeshuka Ligi Kuu na vita iliyobaki ni kucheza mtoano (play off) ambayo kwa mujibu wa msimamo ni timu zaidi ya tano zinaweza kukutana na rungu hilo kutokana na pointi zilizonazo.

KOCHA Mkuu wa Pamba Jiji, Fred Felix ‘Minziro’ ametoa siku 10 kwa wachezaji kabla ya kurejea kujiandaa dhidi ya JKT Tanzania na KMC akizitaja kama ndizo za kukwepa mtego wa kuangukia kucheza mtoano.

Tayari Kagera Sugar na KenGold zilizopo nafasi ya 16 na 15 mtawalia zimeshuka Ligi Kuu na vita iliyobaki ni kucheza mtoano (play off) ambayo kwa mujibu wa msimamo ni timu zaidi ya tano zinaweza kukutana na rungu hilo kutokana na pointi zilizonazo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Minziro alisema ahueni yao kushuka moja kwa moja, lakini sasa wana kazi ngumu kuhakikisha wanapata matokeo mechi mbili zilizobaki ambazo amezitaja kuwa sio rahisi bila kusuka mipango imara.

“Ni kweli nimetoa mapumziko kwa wachezaji siku kumi ili kuweka miili sawa kabla ya kurudi kwenye mikikimikiki kutetea nafasi ya kubaki msimu ujao. Tuna mechi ngumu, tunahitaji kuwa tayari licha ya presha kubwa iliyopo dhidi yetu,” alisema Minziro.

“Baada ya kuifunga KenGold kidogo tumejiweka kwenye nafasi ya kujitetea kushuka moja kwa moja, haina maana tupo kwenye nafasi nzuri bado tunahitaji kusuka mikakati imara ambayo itatutoa kwenye mstari wa hatari kucheza mechi za mtoano, ukiangalia msimamo timu nyingi zipo kwenye hatari.”

Pamba Jiji ipo nafasi ya 12 katika msimamo ikiwa na pointi sawa na Tanzania Prisons ya 13 tofauti ni mabao ya kufungwa, Pamba ina faida ya kumaliza mechi zote nyumbani.