Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mikataba, viwango vyawaondoa nyota 14 Biashara United

Muktasari:

  • Biashara United inajiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu, kombe la Shirikisho la Azam na michuano ya kimataifa barani Afrika baada ya kumaliza katika nafasi ya nne kwenye ligi msimu huu.

TIMU ya Biashara United ya mkoani Mara imeachana na wachezaji wake 14 kwa sababu mbalimbali ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa mashindano ya Ligi Kuu, kombe la Shirikisho na michuano ya kimataifa barani Afrika.

Biashara United ilimaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu msimu huu kwa alama 50 katika mechi 34 nyuma ya bingwa Simba SC, Yanga (nafasi ya pili) na Azam FC (nafasi ya nne) na kufanikiwa kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Nyota waliotangazwa kuachwa na klabu hiyo kupitia taarifa rasmi iliyotolewa Jumapili ni Tariq Simba, Kauswa Bernard, Hassan Mkilindi, Jonathan Zephania, Joseph Ziwa, Ally Mwasomola, Jackson Edward, Baraka Makoba, Angelo Malima, Yusuph Abdullwaheed, Ambrosi Ayoy, Yusuph Jamal, Juma Mpakala na Mushta Batozi.

Akizungumza kwa simu na Mwanaspoti, Katibu Mkuu wa Biashara United, Haji Mtete alitaja sababu za kuachana na nyota hao kuwa ni mikataba kumalizika, kuvunjiwa mikataba kutokana viwango kushuka na matatizo ya nidhamu.

Aliwataja waliomaliza mikataba kuwa ni Mushta Batozi, Yusuph Jamal, Yusuph Abdullwaheed na Jackson Zephania, huku mchezaji Jackson Edward (Isidory) akiachwa kutokana na changamoto ya nidhamu

Mtete aliwataja nyota ambao wamevuniwa mikataba baada ya viwango vyao kuwa chini na kutomrishisha mwalimu kuwa ni Tariq Simba, Kauswa Bernad, Juma Mpakala, Ambrosi Ayoy, Angelo Malima, Jackson Edward, Baraka Makoba, Ally Mwasomola, Hassan Mkilindi na Joseph Ziwa.

"Wengi mikataba yao imekwisha, wengine viwango vyao viko chini havijamridhisha mwalimu kwasababu kuna ambao walisajiliwa na wengine tukawapandisha kutoka timu ya vijana, lakini unakuta tangu aletwe hajacheza hata mechi moja kwahiyo tafsiri yake ni kwamba viwango viko chini," alisema Mtete.

"Tunakwenda kwenye usajili kwahiyo hatuwezi kukaa na watu ambao uwezo (performance) yao haijakaa sawa, Kocha ameona aachane nao watafute changamoto maeneo mengine," alisema.