Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mido Pamba Jiji aingia anga za maafande

Muktasari:

  • Nyota huyo alijiunga na Pamba Julai 19, 2025 kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kuondoka Namungo aliyojiunga nayo katika dirisha dogo la Januari 2025 kwa mkopo pia akitokea Singida, ambapo kwa sasa JKT Tanzania imefungua mazungumzo.

JKT Tanzania imeanza mazungumzo ya kuipata saini ya kiungo mshambuliaji wa Pamba Jiji, Najim Mussa, baada ya mkataba wake wa sasa wa mkopo kutoka Singida Black Stars kufikia tamati mwisho wa msimu huu.

Nyota huyo alijiunga na Pamba Julai 19, 2025 kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kuondoka Namungo aliyojiunga nayo katika dirisha dogo la Januari 2025 kwa mkopo pia akitokea Singida, ambapo kwa sasa JKT Tanzania imefungua mazungumzo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Najim alisema ni mapema kuzungumzia timu atakayocheza msimu ujao, kwani malengo ni kumaliza mechi zilizobaki, licha ya kwamba ana ofa mbalimbali ambazo ameanza kuzipokea kwa siku za karibuni.

"Ni kweli kuna ofa mbalimbali, lakini hata waajiri wangu wa sasa ambao ni Pamba Jiji wananihitaji pia. Sijafanya uamuzi wowote kwa sababu ni mapema na ninaangalia timu nzuri zaidi nitakayoona kwangu itanifaa maishani mwangu," alisema Najim.

Hata hivyo, licha ya kauli hiyo, lakini Mwanaspoti linajua Najim ni miongoni mwa viungo wanaopigiwa hesabu ya kutua katika kikosi cha maafande wa JKT Tanzania ambao wameonyesha nia ya kumhitaji kutokana na kiwango chake.

Nyota huyo alisajiliwa na Singida 2024-2025 akitokea Tabora United ambayo sasa ni TRA United, japokuwa uwepo wa viungo wakiongozwa na Josaphat Bada anayeichezea JS Kabylie ya Algeria msimu huu ulichangia yeye kuondolewa.

Viungo wengine waliosababisha mchezaji huyo kushindwa kupata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza cha Singida Black Stars licha ya kiwango bora alicho nacho akiwa na TRA United ni Emmanuel Keyekeh na Mohamed Damaro ambaye kwa sasa anaichezea Yanga.