Michuano ya Chalenji yasogezwa Desemba
Muktasari:
Mashindano hayo yalitarajiwa kuanza Novemba 25 hadi Desemba 9 lakini sasa yataanza Desemba tatu hadi 17 nchini Kenya katika kaunti za Kakamega, Kisumu na Nakuru japo Nairobi na Machakos zimetengwa kama mbadala iwapo hali ya anga itakataa kaunti husika.
Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limesogeza mbele mashindano ya kombe la Chalenji.
Mashindano hayo yalitarajiwa kuanza Novemba 25 hadi Desemba 9 lakini sasa yataanza Desemba tatu hadi 17 nchini Kenya katika kaunti za Kakamega, Kisumu na Nakuru japo Nairobi na Machakos zimetengwa kama mbadala iwapo hali ya anga itakataa kaunti husika.
Mataifa 12 yanatarajiwa kushirikishwa huku Libya na Zimbabwe yakialikwa kuchukua nafasi za Djibouti na Eritrea.
Kikosi cha Harambee Stars kilinyakua taji hili mwaka 2013 mara ya mwisho Kenya kuandaa mechi hizi wakiwalaza Sudan 2-0 ugani Nyayo shukrani kwa magoli yake straika Allan Wanga.
Nchi za Kenya, Tanzania, Uganda, Somalia, Sudan, Ethiopia, Sudan Kusini, Zanzibar, Burundi na Rwanda pia zitakazoshiriki.
Hata hivyo, mwandishi wa MCL Digital anafahamu kuwa mashindano haya yamesogezwa mbele kwa sababu ya wafadhili kukosa fedha.