Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Messi vs Ronaldo : Siku ya kuzaliwa kwa Messi yawa gumzo

Muktasari:

Na ingawa soka ni mchezo wa kitimu, mara nyingi wachezaji mmoja mmoja mastaa ndio wanaokuwa kivutio katika mijadala. Ronaldo ana wafuasi wengi katika akaunti yake ya Facebook kuliko akaunti ya Facebook ya klabu yake ya Real Madrid (hata hivyo kwa sasa Ronaldo anaichezea Juventus) watu 91 milioni zaidi.

KATIKA toleo lililopita, mwandishi, Luca Caioli alionyesha jinsi ambavyo Ronaldo yuko juu kwenye mitandao na wakati mwingine kuizidi klabu aliyoikuwa akiichezea Real Madrid kwenye Facebook. Sasa endelea…

Mitandao ya kijamii ni jukwaa huru ambako kila mtu anakuwa na uhuru wa kutoa maoni na soka ndio mchezo ambao unaongoza katika mijadala ya kwenye mitandao.

Na ingawa soka ni mchezo wa kitimu, mara nyingi wachezaji mmoja mmoja mastaa ndio wanaokuwa kivutio katika mijadala. Ronaldo ana wafuasi wengi katika akaunti yake ya Facebook kuliko akaunti ya Facebook ya klabu yake ya Real Madrid (hata hivyo kwa sasa Ronaldo anaichezea Juventus) watu 91 milioni zaidi.

Katika mtazamo huo, Messi yuko kivingine kabisa ana watu milioni 86 wanaofurahia na kuvutiwa (likes) na anachoandika kwenye Facebook na hivyo kuwa na idadi ndogo ukilinganisha na klabu yake ya Barcelona yenye watu 94 milioni kama ilivyo kwa Cristiano Ronaldo.

Na ingawa si kawaida ya Messi kujitokeza na kuanika mambo makubwa makubwa kupitia mitandao ya kijamii bado ni mwenye kufahamu ukweli kwamba linapokuja suala la kibiashara kwenye soka duniani, mitandao ya kijamii ina nafasi yake muhimu na ya kipekee katika mambo ya promosheni.

Kama ilivyo kwa Ronaldo, Messi naye kuna wakati anatupia picha zake na familia yake na wachezaji wenzake, ni ama anapokuwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo au anapotangaza baadhi ya mambo na wadhamini wake.

Wachezaji wote hao, Messi na Ronaldo pia wapo makini au wanajitokeza katika mitandao ya Instagram na You Tube na eneo hilo kwa mara nyingine, Ronaldo yuko mbele.

Pamoja na kwamba Messi si mwenye kujishughulisha kwa sana kwenye mitandao ya kijamii lakini ananufaika nayo pamoja na klabu yake ambayo humsaidia kumpaisha ili naye aweze kuwa juu katika eneo hilo.

Kwa mfano Juni, 24, 2015 wakati Messi akisherehekea miaka 28 ya kuzaliwa kwake, klabu yake ya Barcelona au Barca iliwataka mashabiki kumkumbuka Messi katika siku hiyo kwa mapicha.

Nia ya klabu ya Barcelona ilikuwa ni kuifanya siku hiyo ya kuzaliwa kwa Messi liwe tukio kubwa duniani kote na kwa kuangalia jinsi matokeo yalivyokuwa, tukio hilo lilikuwa na mafanikio makubwa.

Mashabiki kupitia mitandao waliifanya siku hiyo kuwa kubwa na gumzo la kipekee, ‘walirushiana’ picha za video maarufu na zenye mvuto za Messi zikiwamo za mabao yake bora, picha zake akiwa mdogo au picha nyingine akiwa na mataji mbalimbali pamoja na rekodi zake. Kauli za kumtakia mafanikio zilimiminika kwa lugha mbalimbali za kimataifa zilizoeleweka.

Katika ripoti za vyombo vya habari, gazeti maarufu nchini Hispania la El Mundo lilidai kwamba Messi na Ronaldo ni aina ya kundi la watu wachache mastaa ambao wameufanya utawala wa mitandao yao ya kijamii kuwa chini ya maprofesheno.

Na hata sifa na mafanikio yao imekuwa sehemu muhimu ya mbinu za mawasiliano, hakuna kinachoachwa na hilo linaweza kuelezewa kupitia namna Ronaldo anavyopaa kwenye mtandao wa Facebookna Twitter hususan mara baada ya kubeba tuzo ya Ballon d’Or.

Tukio hilo halikuachwa lipite hivi hivi, kundi la wataalam wa mawasiliano ya umma lililomzunguka likaingilia kati na kuweka mambo sawa kuanzia mwaka 2015. Amekuwa akitupia matukio mengi yanayomhusu na kuonekana kama yuko macho kila wakati akijua kinachoendelea.

Itaendelea Jumanne ijayo…