Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Messi vs Ronaldo : Ronaldo aifunika hadi Real Madrid kwenye Facebook

Muktasari:

Msingi wa mafanikio ambayo Ronaldo amekuwa akiyapata kwa kuvutia watu wengi kwenye mitandao ya kijamii ni utayari wake wa kushirikisha watu katika matukio mbalimbali yake binafsi pamoja na mafanikio yake kwenye soka.

KATIKA toleo lililopita, mwandishi, Luca Caioli alielezea jinsi mchuano wa mastaa ulivyo katika mitandao ya kijamii akionyesha namna Cristiano Ronaldo alivyo mbali katika eneo hilo hadi kuanzisha website ya vivaronaldo.com, Endelea…

“Tumepata uzoefu ambao umetupa hamasa kuwapa fursa wafuasi wa kipekee wa Ronaldo kwa miaka miwili na nusu, mnaweza kuendelea kumuunga mkono Ronaldo kupitia Viva Ronaldo kwenye akaunti za Facebook, Twitter na Instagram.

“Asanteni kwa kuwa mashabiki bora duniani! Subirini ujio wa kilicho bora ambacho tunaendelea kukifanyia kazi, tunachokiandaa kitaendelea kuwapa myapendayo kuliko ilivyokuwa awali,’’ ilisema taarifa hiyo.

Msingi wa mafanikio ambayo Ronaldo amekuwa akiyapata kwa kuvutia watu wengi kwenye mitandao ya kijamii ni utayari wake wa kushirikisha watu katika matukio mbalimbali yake binafsi pamoja na mafanikio yake kwenye soka.

Zaidi ni kuhusu ile tabia yake binafsi na si katika mbinu za kibiashara, labda ni kwa sababu hiyo ndiyo maana Messi ambaye si mtu wa kuyaanika maisha yake binafsi na hivyo huwezi kumlinganisha na Ronaldo linapokuja suala la kuchuana kwenye mitandao ya kijamii.

Kuna akaunti maalum ya Twitter ya ‘Team Messi’ ni akaunti ambayo ilianzishwa na inasimamiwa na wadhamini wa Messi yenye watu wanaoisoma zaidi ya milioni 1.7 lakini hadi wakati huo hakuwa na akaunti Twitter.

Na wakati mwingine ni familia yake ndiyo inayotumia akaunti za Twitter kwa ajili ya kujibu hoja mbalimbali au kukanusha madai yanayotolewa na watumiaji wengine wa Twitter kumhusu Messi.

Ni kama ambavyo dada yake aliwahi kutumia akaunti ya Twitter kwa kusema, “Ujumbe kutoka kwa Leo, “kwa mara nyingine napenda kufafanua kuwa sina akaunti ya Twitter na sina mpango wa kuwa nayo kwa sasa na kama nitaamua kuwa nayo nitatangaza kupitia akaunti yangu ya Facebook.”

“Naamini huu ni ufafanuzi wa kutosha ili watu wasipotoshwe kupitia akaunti yoyote ambayo ina jina langu.”

Lakini yuko Messi mwingine kwenye Twitter, “Matias Messi, kaka yake Messi, Twitter zake ambazo amekuwa akizituma mtandaoni zimekuwa zikisababisha mkanganyiko kwa mashabiki wa soka.

Baadhi ya mashabiki hao kwa mfano wamekuwa wakihoji kwa nini mashabiki wa Real wamekuwa wakimsoma wakati hawampendi na ingawa alifafanua kwamba hakuwa akiwazungumzia mashabiki wote wa Real. Mjadala tayari ulikuwa umepamba moto.

Pia aliwahi kuibua taharuki alipoamua kumlinganisha Ronaldo na Messi kwa kutoa habari kwenye Twitter kwa kuweka michoro ya mataji ya mwaka 2009 akidai kwamba alifanya hivyo kwa lengo la kumuunga mkono Messi na familia yake.

Mitandao ya kijamii ni dhahiri kwamba ni eneo jingine la mashindano kati ya mastaa na watu maarufu au kwa mashabiki wao duniani kote. Ni mpambano wa dunia nzima ambao hauonyeshi dalili zozote za kupungua.

Ni mpambano ambao kwa kawaida huanza kabla ya mechi au kabla ya tuzo kutolewa kama vile Ballon d’Or na mpambano huwa mkali hasa wakati wa pambano la mahasimu hasa wachezaji wanapojikuta katika kushutumiwa kusikokwisha.

Hapo kunakuwa na ushuhuda wa mapenzi ya dhati na chuki katika uchambuzi, maoni, na machapisho mbalimbali katika namna ya kuunga mkono na kupinga.

Mitandao ya kijamii ni jukwaa huru ambako kila mtu anakuwa na uhuru wa kutoa maoni na soka ndio mchezo ambao unaongoza katika mijadala ya kwenye mitandao.

Na ingawa soka ni mchezo wa kitimu, mara nyingi wachezaji mmoja mmoja mastaa ndio wanaokuwa kivutio katika mijadala.

Ronaldo ana wafuasi wengi katika akaunti yake ya Facebook kuliko akaunti ya Facebook ya klabu yake ya Real Madrid (hata hivyo kwa sasa Ronaldo anaichezea Juventus) watu 91 milioni zaidi.

Itaendelea Jumanne ijayo…