Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mechi tatu za kimkakati Mbeya Kwanza

MBEYA KWANZA Pict

Muktasari:

  • Msimu huu kikosi hicho kiko nafasi ya nne na pointi 57, nyuma ya Kagera Sugar iliyokusanya pointi 65, ikiwa ya pili na vinara, Geita Gold yenye 68 na timu hiyo iliyocheza mechi 27 hadi sasa, imeshinda 18, sare tatu na kupoteza sita.

KOCHA Mkuu wa Mbeya Kwanza, Maka Mwalwisi amesema mechi tatu za mwisho ndizo zitakazoamua hatima ya kikosi hicho msimu huu, japo kuna mikakati mizuri aliyoweka na wachezaji wa timu hiyo ili kuhakikisha wanafanya vizuri na kutimiza malengo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mwalwisi amesema katika mechi tatu zilizobakia anakutana na timu mbili zenye malengo sawa na ya kikosi hicho kwa maana ya kupigania nafasi ya kucheza Ligi Kuu kwa msimu ujao, jambo linaloongeza mvuto wa ushindani.

"Katika mechi tatu za mwisho moja tutacheza nyumbani na mbili tutakuwa ugenini, tunakutana na timu zenye malengo tofauti tofauti, japo miongoni mwa mikakati yetu ni kucheza kwa tahadhari kuhakikisha tunaepuka mitego yao," amesema Mwalwisi.

Kocha huyo wa zamani wa Ihefu kwa sasa Singida Black Stars, licha ya uzoefu mkubwa alionao wa kufundisha timu mbalimbali ikiwemo TMA ya Arusha, ila ana kazi ya kuipigania Mbeya Kwanza irejee tena Ligi Kuu baada ya kushuka msimu wa 2021-2022.

Katika mechi tatu zijazo, Mbeya Kwanza itaikaribisha Stand United 'Chama la Wana' Juni 7, kisha kuifuata Polisi Tanzania Juni 14, huku ikihitimisha msimu wa 2025-2026 kwa kucheza dhidi ya Kagera Sugar inayopigania kurejea tena Ligi Kuu Bara.

Msimu huu kikosi hicho kiko nafasi ya nne na pointi 57, nyuma ya Kagera Sugar iliyokusanya pointi 65, ikiwa ya pili na vinara, Geita Gold yenye 68 na timu hiyo iliyocheza mechi 27 hadi sasa, imeshinda 18, sare tatu na kupoteza sita.