Mechi Simba, Mbeya Kwanza haieleweki
Muktasari:
LEO jioni katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi kulikuwa na mechi ya kirafiki kati ya Simba dhidi ya Mbeya Kwanza kutokea Ligi Daraja La Kwanza.
LEO jioni katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi kulikuwa na mechi ya kirafiki kati ya Simba dhidi ya Mbeya Kwanza kutokea Ligi Daraja La Kwanza.
Mechi hiyo ilipangwa kwa ajili ya Simba kujindaa na mchezo wa kombe la Shirikisho (ASFC), wakati Mbeya Kwanza wao wakiwa katika maandalizi ya Ligi Kuu Bara msimu ujao.
Taarifa kutoka ndani ya kikosi cha Mbeya Kwanza ambao wamepanda Ligi Kuu Bara msimu huu zilieleza kuwa wanatambua mchezo huo upo pale pale na utapigwa muda uliopangwa.
"Tunafahamu mechi ipo. hatuna taarifa ya kuhairishwa kwa mchezo. Tupo katika hatua za mwisho kwenye maandalizi yetu kabla ya kwenda Azam Complex kuwakabili Simba," amesema mtoa taarifa huyo.
Kwa upande wa Simba wao kwanza wachezaji na benchi la ufundi wametawanyika kila mmoja yupo kwake kwa ajili ya mapumziko siku ya leo.
"Sina taarifa ya kucheza mechi yoyote ya kirafiki jioni ya leo kwanza nipo nyumbani kwangu kwa ajili ya mapumziko ya siku mbili," amesema mtoa taarifa huyo na kuongezea;
"Kama kuna mechi ya kirafiki hilo wao ndio wanafahamu lakini kwa upande wetu ratiba inaonyesha tunakutana kesho jioni."
Mmoja wa wachezaji wa kikosi cha Simba, alisema hakuna mchezo wa kirafiki kwani kila mchezaji yupo nyumbani kwake kuendelea na ratiba zake nyingine.
"Hatuna taarifa ya mechi na ratiba ambayo tunayo wachezaji kesho jioni ndio tutakuwa na mazoezi katika uwanja wetu wa Mo Bunju Arena," alisema mchezaji huyo.
Kocha wa kikosi cha Mbeya Kwanza, Michael Mnyali alisema hawana ratiba ya kuondolewa kwa mechi hiyo na wapo katika hatua za mwisho kuelekea uwanjani.
"Tunachofahamu mechi yetu na Simba bado ipo pale pale na hakuna mabadiliko yoyote," amesema Mnyali.