Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchengerwa: Nendeni mkaishangilie Simba, Afrika Kusini ni salama

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa

Muktasari:

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amewatoa hofu mashabiki wa soka wanaotaka kwenda Afrika Kusini kuishangilia Simba katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates kuwa watakuwa salama.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amewatoa hofu mashabiki wa soka wanaotaka kwenda Afrika Kusini kuishangilia Simba katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirateskuwa watakuwa salama.

Mchengerwa ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Aprili 21, 2022 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

"Niseme tu kwamba sisi kama Serikali tunafuatilia kwa karibu usalama wa timu na hivi ninavyoongea nimemteua msaidizi wangu Mkurugenzi wa Michezo ili aweze kuniwakilisha kusimamia hili" amesema Mchengerwa

Amesema Watanzania na Waafrika Kusini ni ndugu wa muda mrefu hivyo ni mategemeo kuwa hakutakuwa na jambo lolote linaloweza kuhatarisha usalama.

Ameeleza kuwa katika mechi hiyo Simba inakwenda kushindana siyo kushiriki ili kuliwakilisha taifa ambapo amewataka wachezaji kucheza kwa weledi na ari ili ipige hatua katika hatua inayofuata hatimaye ilete kombe nyumbani.

Akizungumzia kuhusu kuzisaidia timu za Taifa, Mchengerwa amesema tayari Serikali imeshatoa fedha kwa ajili ya kufanya maandalizi kwenye kambi zote za timu hizo.

Amesema dhamira ya taifa ni kushiriki kwenye Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) na kuratibu mashindano hayo hapa hapa nchini.

Amesema tayari Serikali inafanya maandalizi hayo kwa kuandaa timu bora zitakazofuzu na kuandaa miundombinu ya michezo hiyo.

Katika hatua nyingine, Mchengerwa amesema kutokana na kuendelea kufanya vizuri, Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi nane Afrika ambazo kombe la dunia litapita ambapo hapa nchini linatarajia kufika mwisho wa mwazi huu.