Mayele anyanyua nyomi Arusha

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele amepokelewa kwa shangwe na mashabiki wa soka mkoani Arusha alipokuwa akitoka ndani ya vyumba vya kubadilisha nguo kuingia uwanjani kwa ajili ya kupasha misuli.
Mayele ametokea ndani ya vyumba kuelekea uwanjani, kujiandaa na mechi yao ya kwanza ya ufunguzi wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Polisi Tanzania unaotarajiwa kupigwa
Mayele ambae ndio mfungaji tegemezi wa klabu ya Yanga, nyota yake imezidi kung'aa baada ya juzi mechi ya Ngao ya hisani kufanikiwa kuingiza kambani mawili yaliyoifanikisha timu yake kutwaa ishindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba.
Akitoka katika vyumba vya kubadilishia nguo, Mayele alionyesha ishara ya kupunga mkono hali iliyoibua furaha kwa mashabiki walioitikia kwa kupunga mikono huku wakisimama na kiliita jina "Mayele, Mayele, Mayele" huku wengine wakionyesha ishara ya kutetema.
Kikosi Cha Yanga Kiko Arusha kwenye uwanja wa sheikh Amri abeid kumenyana na timu ya Polisi Tanzania ikiwa Ni mechi ya awali ya ligi kuu Tanzania bara.