Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mayele ana jambo lake, Simba nao wapo

Mayele ana jambo lake Bara

SIMBA bado ina kidonda cha kufungwa mabao 2-1 na Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii, Agosti 13 lakini kana kwamba haitoshi, mabao mawili ya mshambuliaji Fiston Mayele kwenye mechi hiyo yamewaongezea kidonda kingine.

Mabao hayo mawili ya Mayele kwenye mechi ya Ngao ya Jamii yameifanya Simba kuwa miongoni mwa timu zilizofungwa idadi kubwa ya mabao kwenye mechi za kimashindano na mshambuliaji huyo nyota wa Yanga tangu alipoanza kuitumikia timu hiyo msimu uliopita.

Tangu Mayele alitua Yanga, ameifungia jumla ya mabao 22 katika mechi alizocheza za Ligi Kuu ya NBC, Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na Ngao ya Jamii.

Katika mabao hayo Simba pekee ameifunga mabao matatu katika mechi tano alizokutana nazo, ikiwa ndio idadi kubwa ya mabao kuifunga timu moja sawa na 13.6% ya mabao yote aliyofunga straika huyo tangu alipoanza kuitumikia Yanga.

Na mabao hayo matatu aliyoifunga Simba, ameyapata katika mechi za Ngao ya Jamii mara ya kwanza ikiwa ni msimu uliopita alipopachika bao pekee na wikiendi iliyopita kufunga mawili.

Mbali na Simba, Mayele pia amefunga mabao matatu Coastal Union na Biashara United.

Kiujumla, tangu Mayele alipoanza kuitumikia Yanga, amezifunga timu 13, Simba, Polisi, KMC, Geita Gold, Biashara, Coastal, Azam, Namungo, Kagera Sugar, Mbao, Mbeya Kwanza, Dodoma Jiji na Mtibwa Sugar.

Timu za Azam, Kagera na Mbeya Kwanza kila moja amezifunga mabao mawili huku zilizobakia nyingine akizifunga bao moja moja.