Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mavugo katua mwanangu!

Muktasari:

  • Straika huyo mwenye mabao mawili mpaka sasa katika ligi ya msimu huu ameonyesha kurejesha makali yake akimfunika John Bocco mazoezini.

KAMA kuna watu wanambeza Laudit Mavugo, basi imekula kwao, kwani straika huyo Mrundi kwa tizi alilokuwa akilipiga kwenye mazoezini ya timu hiyo kujiandaa na mchezo wao wa Jumapili, linaonyesha wazi amerudi kwenye fomu.

Simba inaifuata Mbeya City leo Ijumaa kwa ndege, ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza pointi mbili muhimu mbele ya watani zao Yanga Jumamosi iliyopita, lakini jinsi Mavugo alivyojinoa ni kama ametuma salamu Mbeya.

Simba ilikuwa ikifanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini chini ya makocha Joseph Omog na msaidizi wake Masudi Djuma.

Tangu Jumatatu wiki hii Simba ilipoanza tizi kujiandaa na pambano lao la Mbeya City, mwandishi aliweka kambi na kushuhudia vinara hao wa Ligi Kuu Bara wakipiga mazoezi ya kufa mtu.

Hata hivyo katika mazoezi hayo imethibitika kuwa, straika Laudit Mavugo anarudi baada ya kuyumba tangu atue Msimbazi akitokea Vital' O ya Burundi.