Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashujaa yaanza na straika wa Stand United

Muktasari:

  •  Mshambuliaji huyo wa zamani wa Mbao, Mgambo Shooting na Dodoma Jiji, akiwa na Stand United msimu huu ameifungia mabao nane na assisti tano, ambapo saba ameyafunga kwenye ligi na moja kwenye kombe la Shirikisho la Azam

TIMU ya Mashujaa FC imeanza kufanya maboresho katika kikosi chake kwenye dirisha dogo la usajili ikianza kwa kumsajili mshambuliaji wa Stand United ya Shinyanga, Emmanuel Mtumbuka.

Mtambuka ambaye ni usajili wa kwanza wa timu hiyo kwenye dirisha hili ameingia makubaliano na Mashujaa ya mkataba wa mwaka mmoja, ambapo amekuwa akiwindwa na timu mbalimbali ikiwemo JKT Tanzania.

Mshambuliaji huyo ambaye alikuwa kinara wa mabao wa Stand United akiwa amefunga mabao saba na asisti tano kwenye Ligi ya Championship, anakwenda kuongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji la Mashujaa ambalo limekuwa butu.

Mashujaa inakamata nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi tisa baada ya kucheza michezo 12 ikiwa imeshinda miwili, sare tatu na kupoteza saba, huku ikifunga mabao tisa na kuruhusu 17.

Timu hiyo imemtambulisha leo Mtumbuka kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ikisindikiza na maneno: “Tumemnasa Mshabuliaji wa boli Emmanuel Mtumbuka kutoka Stand United.

“Namba haziongopi mwamba anafunga na kutengeneza nafasi kwelikweli. Huku ndipo panakufaa shujaa, karibu uwatumikie Watanganyika,” imesema taarifa hiyo

Akizungumza na Mwanaspoti, Mtumbuka amesema ni furaha kujiunga na Mashujaa huku akiwa anarejea Ligi Kuu kwa mara ya pili baada ya kufanya hivyo akiwa na Mbao ya Mwanza, ambapo ameahidi kushirikiana na wenzake kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri na kutoka mkiani.

“Nashukuru mwalimu (Mohamed Baresi) amenipokea vizuri yeye na wasaidizi wake wameniona mazoezini na kunikubali kwahiyo nitashirikiana na wenzangu waliopo kuisaidia timu. Mashabiki wasiikatie tamaa timu yao tutapambana kufanya vizuri,” amesema Mtumbuka