Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashujaa, JKT TZ zafukuzia saini ya Sure Boy

SURE BOY Pict

KIUNGO mkabaji aliyemaliza mkataba wake na Yanga, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ imeelezwa anatakiwa na timu mbalimbali za Ligi Kuu ya NBC ikiwemo JKT Tanzania na Mashujaa.

Sure Boy alijiunga na Yanga Januari Mosi, 2022 akitokea Azam.

Mwanaspoti limepata taarifa kwamba, timu hizo zinazohitaji huduma yake kitu kikubwa wanachoshawishika nacho kutoka kwa mchezaji huyo ni uwezo wake na uzoefu alionao. Chanzo cha ndani kutoka Mashujaa kilisema: “Yanga amekosa nafasi ya kucheza, lakini akicheza mara kwa mara anaweza akafanya vitu vikubwa na akawa msaada mkubwa katika timu.”

SURE 01

Kwa upande wa JKT Tanzania, kilisema: “Kukosa nafasi katika timu moja siyo kuanguka kwa kiwango cha mchezaji, bado tuna imani kubwa na kiungo huyo endapo tukifanikiwa kumpata ataongeza kitu kikosini.”

Katika eneo la kiungo mkabaji ndani ya Yanga, Sure Boy alikuwa akisubiri mbele ya Khalid Aucho, alipoondoka, akaendelea tena kutopewa nafasi kubwa akicheza Duke Abuya aliyemaliza na mabao mawili na asisti saba na Mohamed Damaro.

SURE 02

Alipotafutwa meneja wake, Herry Mzozo amesema: “Sure Boy kwa sasa ni mchezaji anayeweza kucheza timu yoyote na akafanya vizuri, ligi ndiyo kwanza imeisha, hivyo hatuwezi kusema anaenda wapi.”