Masaka apona, aanza kukiwasha

NYOTA wa timu ya Wanawake ya Tanzania 'Twiga Stars' ambaye anacheza soka la kulipwa huko BK Hacken nchini Sweden rasmi amepona majeraha ya goti yaliyokuwa yanamsumbua kwa muda mrefu.
Masaka ambaye amejiunga  na Hacken akitokea Yanga Princess April mwaka huu alifanyiwa upasuaji wa goti Mei mwaka huu  na ikamlazimu kukaa nje kwa miezi miwili kabla ya kurudi tena uwanjani mwishoni mwa mwezi uliopita.
Kwa mara ya kwanza Masaka alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na timu hiyo Julai, 30 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Valerenga  inayoshiriki Ligi Kuu nchini Norway.
Mchezo huo ambao ulipigwa nchini Sweden ulimalizika kwa timu ya Masaka kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 ambayo licha ya Aisha kutofunga alionyesha kiwango bora sana.