Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Manara aibua jambo dhidi ya Senzo

HAJI Manara, aliyekuwa ofisa habari wa Simba amedai kuwa mtendaji mkuu wa zamani wa Simba, Senzo Mbatha aliajiriwa ili amfukuze kazi.

Haji alibwaga manyanga ndani ya Simba baada ya kutokuwa na maelewano mazuri na mabosi wa klabu hiyo.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo, Manara amedai kuwa alipoletwa Mbatha kutoka Afrika Kusini aliniita ofisini na kuniambia kwamba waajiri wamemwambia kazi yake ya kwanza ni kumfukiza yeye.

"Senzo aliniita ofisini akaniambia kwamba kazi ya kwanza ambayo amepewa na mabosi waliomuajiri ni kumfukuza kazi yeye jambo ambalo yeye alilikataa," amedai Manara.

"Mbatha aliniambia kwamba hakuona maana ya kunifukuza kwa kuwa alikuwa hajafanya nami kazi na aliona ile Simba Day ya 2019, hivyo ni mtu muhimu.

"Nilibaki Simba ila kwa kuwa ilikuwa hivyo nikafanya naye kazi kwa ushirikiano na kila kitu kiliendelea mpaka pale ambapo Senzo akaondoka nikajua kwamba anayefuata ni mimi."


IMEANDIKWA NA DAUDI ELIBAHATI