Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mamilioni ya Simba, Yanga yaanza kazi

Simba na Yanga zilivyopambana Jumatano Yanga ilibamizwa 2-1

MWANDISHI WETU MIAMBA mitatu iliyofanya usajili wa mamilioni Simba, Yanga na Azam ni miongoni mwa timu 14 zitakocheza mechi saba za ufunguzi wa Ligi Kuu ya Bara katika viwanja tofauti wikiendi hii. Katika ligi hiyo, ambayo bingwa atapata sh.milioni 40, itakuwa na makocha wanne wa kigeni kutoka England na Uganda, Simba na Yanga zitaanza kazi kesho Jumapili zikipambana na timu zinazomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). Mjini Tanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani uliofanyiwa matengenezo makubwa na uongozi wa Azam FC, Coastal Union ya Kocha Hafidh Badru itacheza na Mtibwa ya Tom Olaba, leo Jumamosi. Kagera Sugar, ambayo haijawahi kuchukua ubingwa wa Bara, iko chini ya kocha mpya Salum Mayanga aliyeikimbia Mtibwa, itacheza na Ruvu Shooting wakati Toto African iko Mwanza ikicheza na Villa Squad, ambayo imeanza kuonyesha dalili zote za kushuka daraja kwa kulia ukata hata kabla filimbi haijalia. Polisi Tanzania chini ya kocha msomi Joseph Kanakamfumu itacheza na African Lyon mjini Dodoma huku matajiri wa Azam FC chini ya makocha Waingereza Stewart Hall na Kally Ongala wakicheza na Moro United katika Uwanja mpya wa Chamazi unaoingiza zaidi ya mashabiki 2000. Simba yenye morali kubwa ikiwa na mastraika watatu wa kigeni na viungo wawili, chini ya makocha wa Uganda, Moses Basena na Richard Amatre itacheza na timu ngeni ya JKT Oljoro mjini Arusha wakati Yanga ikicheza na JKT Ruvu jijini Dar es Salaam. Basena, ambaye huenda akatumia mfumo wa 4-5-2 alisema; "Hatuijui Oljoro na hatuna haja ya kufanya hivyo kwa kuwa tuko imara na tutapambana nayo kwa jinsi itakavyokuja. Tuko imara vya kutosha hatuna haja ya kuwa na wasiwasi." Timbe anayependelea kutumia 4-4-2, alisisitiza kuwa; "Tumepoteza Ngao ya Jamii dhidi ya Simba lakini si sababu, tumeelewa udhaifu wetu tunaanza mapambano mapya, tuko tayari kukabiliana na yoyote yule kutetea ubingwa wetu. Tuna mtazamo chanya na tunajua tunachofanya."