Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo matano mechi ya Azam dhidi ya Yanga

Muktasari:

Kuelekea mchezo huo, mwandishi anakuletea mambo matano (5) ambayo pengine hukuyafahamu hapo kabla yanayozihusu timu hizo mbili kubwa nchini ambazo zimekuwa zikitikisa katika medani ya soka nchini.

Azam FC itaikaribisha Yanga katika mchezo wa kuhitimisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini, Jumamosi, Januari 27.
Kuelekea mchezo huo, mwandishi anakuletea mambo matano (5) ambayo pengine hukuyafahamu hapo kabla yanayozihusu timu hizo mbili kubwa nchini ambazo zimekuwa zikitikisa katika medani ya soka nchini.
1. Hii ni mara ya kwanza kwa Uwanja wa Azam Complex ambao unatumiwa na Azam FC kwa mechi zake za nyumbani katika mashindano mbalimbali, kuandaa mchezo baina ya Azam FC na Yanga. Kabla ya hapo, mechi zote zilizokutanisha timu hizo zilikuwa zikichezwa kwenye Uwanja wa Taifa, hata pale ambapo Azam FC walikuwa wenyeji.
2.Iwapo itaibuka na ushindi au kutoka sare dhidi ya Yanga, Azam FC itakuwa inatimiza siku 243 ilizocheza mechi za Ligi Kuu bila kupoteza mechi kwenye uwanja wake wa nyumbani tangu ilipopoteza mchezo wa mwisho dhidi ya Kagera Sugar, Mei 30 mwaka jana.
3.Iwapo itaibuka na ushindi au kutoka sare dhidi ya Azam Jumamosi, Yanga itaweka rekodi ya kuwa timu iliyokaa kwa muda mrefu zaidi bila kupoteza mechi za mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), zinazochezwa ndani ya Jiji la Dar es Salaam ambapo itatimiza siku 351.
Tangu ilipofungwa na Simba kwa mabao 2-1 kwenye mechi ya Ligi Kuu, Februari 11, 2017 Yanga haijafungwa tena katika Ligi Kuu au kombe la FA katika mechi zilizochezwa ndani ya Dar es Salaam.
4. Paul Peter wa Azam FC ndiye mshambuliaji aliyefunga idadi kubwa ya mabao ndani ya dakika chache kuliko mwingine yeyote nchini.
Mshambuliaji huyo amefunga mabao mawili katika mechi mbili tofauti dhidi ya Singida United pamoja na ile dhidi ya Tanzania Prisons. Mabao hayo ameyafunga katika dakika 23 tu. Katika mechi dhidi ya Singida United alifunga baada ya kuingia dakika ya 84 na katika mechi dhidi ya Prisons alifunga bao moja katika dakika 17 tu alizocheza baada ya kuingia dakika ya 73.
5. Tangu mwaka huu uanze hadi sasa, nyavu za Yanga  zimetikiswa mara moja tu ndani ya dakika 90 katika mashindano yote iliyoshiriki ambayo ni Kombe la Mapinduzi na Ligi Kuu.
Yanga walifungwa bao hilo pekee katika mchezo dhidi ya Mlandege kwenye Kombe la Mapinduzi, Januari 2 mwaka huu.
Wakati nyavu za Yanga zikitikiswa mara moja, Azam wameruhusu mabao mawili tangu mwaka huu ulipoanza ambapo nyavu zao zilitikiswa dhidi ya URA kwenye Kombe la Mapinduzi, Januari 5 kabla ya kuruhusu bao lingine kwenye Ligi Kuu dhidi ya Majimaji, Januari 18.