Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Malone aingia anga za Simba

KLABU ya Simba iko kwenye mazungumzo na CotonSport ya Cameroon ili kupata saini ya beki wa kati, Che Fondoh Malone.

Beki huyo anatajwa kuhitajika na miamba hiyo hapa nchini kwa ajili ya kuongeza nguvu eneo la kati baada ya timu hiyo kuachana na Mohamed Ouattara, huku Joash Onyango akiwa mbioni pia kusepa.

Malone (24) inaelezwa endapo dili hilo litakamilika basi atapewa kandarasi ya miaka miwili ya kuitumikia na iwapo atatua ataungana na Mcameroon mwenzake, Leandre Onana aliyesainishwa miaka miwili akitokea Rayon Sports ya Rwanda aliyoifungia mabao 16 na kuwa kinara wa ligi hiyo.

Mbali na kucheza kama beki wa kati, lakini Malone anamudu kucheza pia beki ya kulia kwa ufanisi na kusajiliwa kwake kunaweza kumpunguzia kazi Shomari Kapombe anayecheza na Israel Mwenda.


Wasifu:

Jina: Che Fondoh Malone JR

Kuzaliwa: Mei 23, 1999

Nchi: Cameroon

Nafasi: Beki wa Kati

Klabu: CotonSport