Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makambo atolewa macho Yanga

Muktasari:

  • Makambo ametua Yanga kuchukua nafasi ya Obrey Chirwa, akiungana na wakali wengine kama Matteo Anthony, Mrisho Ngassa, Amissi Tambwe, Ibrahim Ajibu, Yusuph Mhilu, Yahya Akilimali, Said Mussa na Yohana Mkomola.

KAMA kuna mchezaji mpya wa Yanga mwenye kazi Jangwani basi ni straika, Heritier Makambo ambaye anatupiwa macho na wadau wa soka kutaka kuona ana jipya gani mara itakapoanza Ligi Kuu Bara msimu wa 2018-2019.

Makambo ametua Yanga kuchukua nafasi ya Obrey Chirwa, akiungana na wakali wengine kama Matteo Anthony, Mrisho Ngassa, Amissi Tambwe, Ibrahim Ajibu, Yusuph Mhilu, Yahya Akilimali, Said Mussa na Yohana Mkomola.

Baadhi ya nyota wa zamani akiwamo Zamoyoni Mogella alisema straika huyo ndiye atakayekuwa na kazi kubwa msimu ujao ndani ya Yanga ili kufanya mambo yatakayompa heshima mbele ya mashabiki.

Kocha Kennedy Mwaisabula 'Mzazi' alisema kitu kinachofanya mashabiki wawe na hamu ya kuona atafanya nini Makambo ni kutokana na namna walivyoona uwezo wa nyota waliopo.

"Ujio wa Makambo utakidhi haja ya wale wanaomtazamia kufanya miujiza? Kwa kweli Yanga ingekuwa na pesa nadhani ingeleta wachezaji wengi zaidi, waliopo wajitambua na kuonyesha viwango vyao," alisema.