Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MAKALA: Yanga, Tshishimbi walifunika mbaya

YANGA imevuna pointi tatu muhimu mjini hapa mbele ya wenyeji wao Lipuli, lakini kama kuna kitu ambacho mashabiki wa soka wa mji huu wamekifaidi ni  kuiona timu hiyo baada ya muda mrefu, lakini pia kumshuhudia Papy Tshishimbi.

Asikuambie mtu, mji wa Iringa tangu ilipotua Yanga ulikuwa na shamra shamra za mashabiki wa klabu hizo zilizokutana mjini hapa kwa mara ya kwanza baada ya takribani miaka 17. Ziliumana  Uwanja wa Samora.

Juzi Jumamosi ndio ilikuwa balaa zaidi kwani kuanzia saa moja za asubuhi, mashabiki kutoka mjini Iringa na mikoa jirani ya Mbeya, Njombe walianza kumiminika kwenye Uwanja wa Samora wakinunua tiketi na wengine wakitumia fursa hiyo kuuza jezi.

Huko mitaani tambo mbalimbali za mashabiki huku mastaa kama Papy Kabamba Tshishishi, Ibrahim Ajibu, Obrey Chirwa wakiwa gumzo na kuwapa mzuka waliotaka kuwaona uwanjani baada ya kuwachungulia tu kwenye runinga.

MCHANA BALAA

Ilipofika saa sita mchana mageti yote ya Uwanja wa Samora yalifunguliwa na mashabiki walianza kuingia uwanjani hapo huku tiketi zikiendelea kununuliwa.

Hata hivyo, licha ya mashabiki kujitokeza kwa wingi kuishuhudia mechi hiyo, lakini bado wengine walilazimika kuzuiwa kuingia uwanjani hapo kutokana na uwanja huo kujaa na kukosa sehemu ya kukaa mashabiki hivyo wengi kushindwa kuitazama mechi hiyo pamoja na kununua tiketi, walibaki nazo nje.

YANGA WATATA

Wakati wa timu kuingia uwanjani, timu zote, Yanga na Lipuli zilitumia mlango wa geti kuu linalotumiwa na viongozi huku wakiacha mabasi yao yakiingia yakiwa tupu.

Hata hivyo,  viongozi wa Yanga waliwazuia wachezaji wao kuingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo kwa madai kimepuliziwa dawa inayolenga kuwaathiri wachezaji wao.

Meneja wa Yanga, Saleh Hafidh, alisema; “Hii harufu hatuwezi kuruhusu wachezaji wetu kuingia ndani, watabadilishia nguo nje. Wao wanabisha na kudai ni dawa ya chooni haina athari yoyote, sasa kama ni hivyo basi wachezaji wa Lipuli waje, huku sisi twende chumba kile, kama kweli wanamaanisha wanachokisema.”

Hata hivyo, madai ya Yanga yalipingwa vikali  na Meneja wa Uwanja wa Samora, Lazaro Manila aliyesema kwamba Yanga wamevurugwa na imani za kishirikina, lakini  hakuna ukweli wowote wa madai yao.

“Tatizo soka la Tanzania limewatawaliwa na imani za kishirikina sana na wanachokitafuta hapa ni faini tu hakuna kingine. Nenda viwanja vingi nchini hakuna  vyumba vizuri na vya kisasa kama hivi na hakuna cha dawa wala nini. Asubuhi viongozi wa Yanga na TFF (shirikisho la soka) wameingia wamekagua vyumba vyote na wamesema wameridhirishwa hali ya usafi, halafu hawa hawa wanakuja na madai tofauti.”

MECHI ILIVYOKUWA

Timu zote ziliingia uwanjani na kucheza mpira kwa kasi na kujiamini.

Dakika ya 17 ya mchezo huo, kipa wa Yanga, Youthe Rastand, aliumia baada ya kugongana na mmoja wa mabeki wake na mpira kusimama kwa takribani dakika tatu.

Hata hivyo kipa huyo alishindwa kuendelea na mchezo na na kuomba kufanyika kwa mabadiliko kwa kuingizwa Ramadhani Kabwili na kufanya mashabiki wa Lipuli

waliokuwa wakiungwa mkono na wale wa Simba kushangilia sana.

Hata hivyo kicheko cha mashabiki hao kiligeuka kilio muda mchache baada ya Kabwili kuingia kwani, Tshishimbi alifunga bao akimalizia mpira wa kona ya Geofrey Mwashiuya kushindwa kuokolewa na kipa wa Lipuli, Agathon Anthony.

Lipuli hawakuonesha kutetereka kutokana na kuruhusu bao hilo, waliendelea kucheza mpira safi na kujaribu kufika kwenye lango la Yanga japo washambuliaji wake hawakuwa na mawasiliano na malengo yenye tija kupata ushindi kutokana na kushindwa kuzitumia nafasi walizokuwa wakizipata tofauti na Yanga wao ambao  dakika za 45 za mwanzo hawakuonesha kucheza mpira wa kutisha.

Katika kipindi hicho, Yanga ilipata kona mbili  na Lipuli ilipata moja, huku mwamuzi akiongeza dakika 10 za nyongeza kitu kilichoshangaza.

KIPINDI CHA PILI BALAA

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kucheza kwa mashambulizi, lakini bado Lipuli hawakuwa makini safu ya ushambuliaji na kuruhusu nafasi nyingi za kushambuliwa zaidi na udhaifu wa beki wa Lipuli uliipa nafasi zaidi Yanga na kuruhusu bao la pili.

Bao hilo liliwekwa kiufundi na Pius Buswita katika dakika ya 55 akipokea pasi safi kutoka kwa Obrey Chirwa.

Hata hivyo, kipindi cha pili kilionekana kuwa na matukio kadhaa kwa wachezaji kupewa kadi za njano, ambapo wachezaji wa Lipuli Adam Salamba alizawadiwa

kadi ya njano kwa kumchezea ndivyo Said Makapu na Daniel Michael na Ramadhani Kabwili walipewa kadi kwa kuchelewesha mpira.

Makocha wote walifanya mabadiliko, Yanga ikiwatoa Geofrey Mwashiuya kumpisha Matteo Anthon, huku Lipuli ikiwatoa Seif Rashid, Jamal Mnyate na Mussa Nampaka kuwapisha Anthon Tolla, Zawadi Mauya na Lambele  Jarome.

Katika kipindi hiki mwamuzi aliongeza dakika saba na kulifanya pambano zila la Yanga na Lipuli kuchezwa kwa muda wa dakika 107.

YANGA WALISTAHILI

Kwa namna Yanga iliyopambana jihad Samora kwa hakika walistahili kutoka ushindi huo wa kwanza mjini humo baada ya miaka mingi. Kwani Yanga licha ya kuwakosa nyota wake kadhaa wa kikosi cha kwanza, lakini waliocheza walitekeleza yote ambayo walielekezwa na makocha wao wakiongoza na George Lwandamina.

Bao la Tshishimbi licha ya kuwakuna mashabiki wa klabu hiyo, lakini ni la kwanza kwa Mkongomani huyo, tangu aliposajiliwa Jangwani Agosti mwaka jana na vilevile limechangia kuipa Yanga pointi muhimu zilizoifanya ifikishe alama 31.

Mkongo huyo ndiye aliyeonekana kuibeba Yanga katika pambano hilo na kuwakuna wengi kwa soka lake tamu na pasi zilizowafikia wachezaji wenzake. Ndiye aliyepiga pasi nyingi uwanjani hapo, zikiwa ni zaidi ya pasi 45.

MAKOCHA WANENA

Kocha Matola alisema vijana wake wa Lipuli walishindwa kujua mbinu za wapinzani wao jambo lililowafanya kutumia nafasi walizopata na kuruhusu mabao.

“Nimeona tatizo la mabeki walishindwa kucheza na washambuliaji wa Yanga, lakini pia safu ya ushambuliaji yangu pia haikuwa makini kabisa, japo mwamuzi katunyima penalti ya wazi kabisa, lakini tunakubali tumepoteza mechi hii muhimu kwetu, tunaendelea na maandalizi kwa mechi zijazo’.

Naye Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa alisema  licha ya kupata bao kipindi cha kwanza lakini kipindi cha pili walilazimika kubadili mfumo uchezaji kwa vile tayari Lipuli walikuwa wameshawasoma.

“Ni mbinu tu ambazo tuliziona kwamba wenzetu kipindi cha kwanza watacheza vipi hivyo tukaenda nao, lakini kipindi cha pili tulibadili mfumo jambo lililosaidia kupata bao la pili na kuibuka na ushindi wa pointi tatu muhimu.”