Ligi ya Mabingwa, Shirikisho Afrika kuanza Agosti 12

Mashindano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afika kwa msimu wa 2022/23 yataanza kutimua vumbi Agosti 12, 2022.
Hatua za makundi itaanza Septemba na kumalizika kabla ya Novemba 18, 2022.
Michuano ya mtoano inatarajiwa kuanza Februari, 2023 baada ya mashindano ya CHAN nchini Algeria.
Tanzania inawakilishwa na Yanga, Simba kwenye Ligi ya Mabingwa huku Shirikisho ikisubiri mechi tatu za mwisho.
Kutokana na msimu wa Ligi Kuu ulivyo mpka asasa Yanga anaongoza akifuatiwa na Simba huku nafasi ya tatu mpaka ya tano zikiwa bado hazitabiriki kwa Azam FC, Geita Gold na Namungo.