Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha wa Rwanda majaribuni Dar

Kocha wa Taifa Stars,Mrisho Ngassa akitoa maelekezo ya mwisho kwa Mrisho Ngassa. Stars inacheza na Rwanda leo Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa katika mechi ya kufuzu fainali za CHAN ambayo Rwanda wanajua kwamba Ngasa hatacheza kutokana na majeruhi .

MWANDISHI WETU KOCHA wa Rwanda, Sellas Tetteh hana wasiwasi na kikosi chake lakini ametua Dar es Salaam na kikosi cha wanaume 18 akiamini kuwa mshambuliaji Mrisho Ngassa wa Taifa Stars ni majeruhi na hatacheza leo Jumamosi. Vyombo vya habari vya jijini Kigali Rwanda kwa wiki nzima vimekuwa vikimnukuu kocha wa Stars, Marcio Maximo akisema kuwa Ngassa hatacheza hivyo mbadala wake ni Mussa Hassan Mgosi. Daktari wa Taifa Stars, Juma Sufiani amelihakikishia benchi la ufundi kuwa wachezaji nyota Mrisho Ngassa na Uhuru Suleiman wapo salama kuikabili Rwanda leo Jumamosi katika mechi ya kufuzu fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani(CHAN) jijini Dar es Salaam na kwamba hakuna majerui yeyote. Kocha wa Rwanda ambaye ni raia wa Ghana, ambaye anaanza kibarua chake kipya leo Jumamosi mbele Taifa Stars katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za CHAN 2011, amewahakikishia Wanyarwanda kuwa atapata matokeo mazuri lakini akawaambia mashabiki wasiwape presha kubwa wachezaji. Tetteh, ambaye alikuwa kocha bora wa Afrika mwaka jana, anajulikana kimataifa kutokana na kuiongoza timu ya Ghana ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 kutwaa ubingwa wa Afrika na ule wa dunia mwaka 2009. Katika mechi za kirafiki za kujiandaa Rwanda ilizifunga Electogaz mabao 4-0 na AS Kigali mabao 4-1 zote za Ligi Kuu nchini humo. Kikosi cha Rwanda kilichotua jana Ijumaa ni: Jean Claude Ndoli, Jean Luc Ndayishimiye, Mutesa Mafisango (nahodha), Didier Kapet Kouin, Amani Uwiringiyimana, Kalisa Mao, Jean Mugiraneza, Haruna Niyonzima, Donatien Tuyizere, Jamal Mwiseneza, Jean Claude Iranzi, Tumaine Ntamuhanga, Albert Ngabo, Abuba Sibomana, Yussuf Ndayishimiye, Roger Tchouassi, Emmanuel Sebanani na Dady Birori.