Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha mpya Yanga aibukia Simba SC

KOCHA Msaidizi wa Yanga, Momo Medic

LAMPS COLLIN KOCHA Msaidizi wa Yanga, Momo Medic kesho Jumapili atakuwa akiisoma Simba kwa mara ya kwanza itakapokuwa ikicheza na Lengthens ya Zimbabwe. Mtaalamu huyo wa Serbia anakuja Yanga kumsaidia Kocha Mkuu wa timu hiyo, Kosta Papic, lakini kazi yake ya kwanza itakuwa ni kuisoma Simba kesho Jumapili. Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Serbia jana Ijumaa, mke wa Papic anayeitwa Milka alisema mumewe akiwa na Momo walikuwa wameshaondoka nchini humo. "Papic ameshaondoka hapa, nadhani atakuwa uwanja wa ndege, anakuja huko Tanzania akiwa na Medic, nadhani atafika huko Dar es Salaam Jumamosi saa 12:00 jioni," alisema Milka kwa Kiingereza cha 'kujitahidi.' "Ameniambia nchi yenu ni nzuri sana, nitakuja huko mwaka huu, kuna mambo fulani nafanya hapa, lazima nije nione Mlima Kilimanjaro," alisema mke huyo wa Papic mwenye watoto wawili. Momo kutoka Serbia atatua jijini Dar es Salaam leo Jumamosi kuiwahi Simba ambayo watacheza nayo Jumapili ijayo. Momo, ambaye amewahi kuwa msaidizi wa Kosta Papic katika timu za Enugu Rangers na Enyimba za Nigeria kabla ya kuwa naye tena Orlando Pirates anasifika kwa uwezo mkubwa wa kuisoma timu pinzani. Momo, ambaye mwaka jana alikuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Real Sportive ya Ghana, anakuja kumsaidia Papic ambaye amekuwa bila kocha msaidizi tangu atue Dar es Salaam Oktoba mwaka jana. Papic aliiambia Mwanaspoti kuwa licha ya kumleta Momo, anawaleta pia wachezaji wawili kutoka Ghana na watafika Aprili 12. Yondani, Naftali watia hofu Mwandishi Wetu KOCHA wa Simba, Patrick Phiri amewapa matumaini mashabiki wa timu hiyo kuwa wataifunga Lengthens ya Zimbabwe, kesho Jumapili, ila wachezaji wake Kelvin Yondani 'Vidic' na David Naftali ni majeruhi. "Tunaomba mashabiki waje kutushangilia, kwani tunataka sapoti yao. Wachezaji wote wapo vizuri isipokuwa Naftali na Yondani ambao ni majeruhi," alisema Phiri kutoka Zanzibar jana Ijumaa. Phiri alisema timu hiyo itatua leo Jumamosi kutoka Zanzibar, na hapo ndio atajua hatima ya Yondani kuhusu mchezo huo. Lengthens nao wanatarajiwa kutua leo Jumamosi.