Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha KVZ apiga mkwara Kagame Cup

ESMA Pict

Muktasari:

  • Katika michuano hiyo inayoanza Julai 25 hadi Agosti 8 mwaka huu ikichezwa nchini Rwanda, kundi A linaundwa na APR ya Rwanda, Vipers (Uganda), Gor Mahia (Kenya) na Garde Republicaine (Djibouti), kundi B zipo Simba na Singida Black Stars za Tanzania, Jamus ya Sudan Kusini na Mogadishu City kutoka Somalia.

WAKATI mabingwa wa Ligi Kuu Zanzibar, KVZ wakipangwa kundi C katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Kagame Cup), kocha mkuu wa timu hiyo, Hababuu Ali amesema wamejipinga kushindana badala ya kushiriki pekee.

KVZ katika kundi hilo, ipo na Al Hilal ya Sudan, Rayon Sports kutoka Rwanda na Tusker yenye maskani yake nchini Kenya.

Katika michuano hiyo inayoanza Julai 25 hadi Agosti 8 mwaka huu ikichezwa nchini Rwanda, kundi A linaundwa na APR ya Rwanda, Vipers (Uganda), Gor Mahia (Kenya) na Garde Republicaine (Djibouti), kundi B zipo Simba na Singida Black Stars za Tanzania, Jamus ya Sudan Kusini na Mogadishu City kutoka Somalia.

Akizungumza na Mwanaspoti, kocha huyo amesemaanatambua ugumu wa kundi hilo kwa sababu anaocheza nao wote ni mabingwa Afrika Mashariki.

Alisema, hilo haliwazuii kuonesha uwezo wao wa kupambana akiahidi kufanya vizuri.

“Tunajua tutakuwa na mechi ngumu kutokana na wasifu waliokuwa nao wenzetu, mechi hizi zitatusaidia kujiandaa kwa ajili Ligi ya Mabingwa Afrika,” alisema.

Hababuu amesemamichuano hiyo itakuwa sehemu ya maandalizi yao kwani wana mzigo mzito mbele yao kwa mara ya kwanza.

Amesisitiza kuwa, timu inaenda kupambana kwa ajili ya Zanzibar kwani wapo peke yao ikilinganishwa na nchi nyingine baadhi zipo zilizopata uwakilishi wa timu mbili.

KVZ baada ya kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Zanzibar, msimu ujao itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo kocha Hababuu amesema michuano ya Kagame ni sehemu ya maandalizi ya kufanya vizuri kimataifa.