Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KMC yapewa motisha bao moja Sh500,000

Muktasari:

  • Akizungumza na benchi la ufundi pamoja na wachezaji wa klabu hiyo Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Meridianbet Tanzania Bw. Matina Nkurlu, alisema kwamba lengo la zawadi hiyo ni kutoa motisha lakini pesa hizo zitatumika kutoa msaada kwa jamii.

KMC FC "Kino boyz" inayoshiriki Ligi kuu ya NBC imeahidiwa na Mdhamini wao Mkuu Meridianbet Tanzania kupewa Tsh 500,000/= kwa kila goli ambalo klabu hiyo itapata katika michezo ya ligi kuu iliyosalia lengo ni kutoa motisha kwa wachezaji kupambana zaidi.

Akizungumza na benchi la ufundi pamoja na wachezaji wa klabu hiyo Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Meridianbet Tanzania Bw. Matina Nkurlu, alisema kwamba lengo la zawadi hiyo ni kutoa motisha lakini pesa hizo zitatumika kutoa msaada kwa jamii.

“Meridianbet Tanzania tumeamua kununua kila goli mtakalofunga kwa Tsh Laki Tano kwenye michezo yenu ya Ligi Kuu iliyosalia. Lakini jambo kubwa zaidi kiasi kitakacho patikana kitatumika kurejesha kwa jamii kwa sababu KMC ni timu ya Wanakinondoni na Watanzania wote”

Kwa upande wa Nahodha Emmanuel Nvuyekule ‘Manu’ alipongeza juhudi za Mdhamini wao na hii itawaongezea hamasa ya kuendelea kujituma kwa kufunga magoli mengi.

“Nimshukuru mwenyezi Mungu kwa kuwepo nanyi na kuzipokea taarifa hizi, lakini pia niwashukuru Meridianbet kwa kuja na wazo hili naamini hii itaongeza hamasa na kujituma kwenye timu yetu, Kubwa zaidi ni kwamba tuna muahidi mdhamini wetu kuwa tutafanya vizuri na tutafunga magoli  mengi sana ili kusaidia jamii kwa wingi zaidi”

Hata hivyo mpaka sasa KMC imecheza michezo 25, na imebakiza michezo 5 mkononi kabla ya Ligi kumalizika, kwenye msimamo wanashika nafasi ya 12 wakiwa na pointi 26.

KMC kwa sasa imebakiza mechi na Geita Gold, Dodoma Jiji, Singida Big Stars, Tanzania Prisons, na Mbeya City.