Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KMC, Coastal kazi ipo Dar

Muktasari:

  • MZUNGUKO wa pili wa Ligi Kuu Bara unaendelea leo Alhamis, ambapo KMC itaikaribisha Coastal Union katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam mchezo utakaopigwa kuanzia saa 10:00 jioni.

MZUNGUKO wa pili wa Ligi Kuu Bara unaendelea leo Alhamis, ambapo KMC itaikaribisha Coastal Union katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam mchezo utakaopigwa kuanzia saa 10:00 jioni.

KMC chini ya Kocha Mkuu, Thierry Hitimana imekamilisha maandalizi ya mchezo huo na wachezaji wote wapo tayari kuanza vema mzunguko huo kwa kuhakikisha kwamba wanafanya vizuri katika michezo yote licha ya ushindani mkali uliopo.

Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni ipo nafasi ya 10 ikiwa imekusanya alama 16 imepanga kupambana mzunguko huo wa pili kwa kuwa ni hatua ya kuelekea kumalizika msimu wa 2022/ 2023.

Akizungumzia kuanza kwa mzunguko huo, Hitimana alisema wamejipanga vizuri kutokana na kwamba michezo ya mwisho haikuwa na matokeo mazuri na hivyo changamoto kubwa ilitokana na wachezaji wengi kuwa na majeraha lakini kwa sasa wanne wamesharejea jambo ambalo limeleta matumaini makubwa.

“Tunafahamu kuwa mzunguko wa pili utakuwa na ushindani mkali kutokana na kila timu kuhitaji kufanya vizuri na hivyo tunakwenda kupambana ili tupate matokeo mazuri kwakuwa michezo yote ipo ndani ya uwezo wetu.”

Kuhusu mchezo huo, alisema atawakosa wachezaji wawili Hance Masoud na Emmanuel Mvuyekure ambao bado ni majeruhi na kwamba wengine wapo kwenye ari na morali nzuri hivyo kila mmoja yupo tayari kutumika kwa ajili kupata alama tatu.

“Coastal Union ni timu nzuri hata ukiangalia katika mchezo wake wa mwisho ilipata ushindi ikiwa ugenini, lakini hatuliangalii hilo kama changamoto badala yake tunajiandaa kwa ajili kuhakikisha kuwa tunatumia vizuri uwanja wetu wa nyumbani,” alisema Hitimana.