Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo Mkenya aziingiza vitani Simba, Yanga

Muktasari:

  • Inaelezwa kuwa timu za Simba Queens na Yanga Princess zimeanza kumuwania kiungo fundi wa Kenya Police Bullets ya Kenya Diana Wacera.

WAKATI dirisha la usajili likisubiriwa kwa hamu kufunguliwa, tayari timu za Ligi Kuu ya Wanawake zimeanza kufanya usajili mapema kuelekea msimu mpya.

Inaelezwa kuwa timu za Simba Queens na Yanga Princess zimeanza kumuwania kiungo fundi wa Kenya Police Bullets ya Kenya Diana Wacera.

Mkataba wa kiungo huyo na klabu ya Police Bullets, unatamatika mwishoni mwa msimu huu na inaelezwa bado hajasaini mkataba mpya hivyo atakuwa huru kuchagua wapi anakwenda.

Hadi sasa inaelezwa Yanga imevutiwa zaidi na mchezaji huyo lakini ni kama Wacera anavuta muda kuangalia timu ipi itaongeza mkwanja ili amwage wino.

Hata hivyo, matakwa makubwa ya mchezaji ni kucheza Simba Queens ili abebe ubingwa na kucheza michuano ya kimataifa ambayo itampa soko kubwa la kuonekana.

"Bado hajasaini anaangalia timu ipi ni sehemu sahihi kwake ameongea na baadhi ya Wakenya wenzake wanaocheza hapa amevutiwa zaidi na Simba kutokana na mafanikio makubwa ya timu hiyo," kilisema chanzo hicho.

"Lakini pia pesa ni kipaumbele kingine kwa hiyo kama atashawishiwa na vitu hivyo huenda akasaini timu mojawapo lakini matamanio yake makubwa Simba ila ngoja tuone mwishoni mwa msimu itakuwaje."

Simba Queens msimu huu imesema itafanya marekebisho baadhi ya maeneo ikiwemo la kiungo wa kati ambalo limekuwa changamoto hivyo kama itampata nyota huyo huenda ikaziba pengo hilo.