Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kissu aanika mikakati mipya Polisi Tanzania

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti, Mapigano alisema licha ya kutoanza msimu na kikosi hicho ila kitendo cha kusajiliwa kwake ni heshima kubwa, huku akiweka wazi atahakikisha malengo ya timu hiyo ya kutaka kurejea tena Ligi Kuu Bara anayapigania.

BAADA ya kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na maafande wa Polisi Tanzania, aliyekuwa kipa wa Biashara United, David Kissu Mapigano amesema moja ya mikakati yake ni kuhakikisha anakipambania kikosi hicho kupanda Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mapigano alisema licha ya kutoanza msimu na kikosi hicho ila kitendo cha kusajiliwa kwake ni heshima kubwa, huku akiweka wazi atahakikisha malengo ya timu hiyo ya kutaka kurejea tena Ligi Kuu Bara anayapigania.

“Nimeamua kutafuta changamoto mpya na nashukuru kwa nafasi niliyoipata hapa, Ligi ya Championship ni ngumu hasa michezo hii ya mzunguko wa pili, ila naamini tukishirikiana sisi wachezaji wenyewe, viongozi na benchi la ufundi tutafanikiwa.”

Kipa huyo aliyezichezea timu mbalimbali zikiwemo za Simba, KMC FC, Namungo na Azam FC za Tanzania na Gor Mahia ya Kenya, amejiunga na maafande hao akiungana na kiungo, Rehani Kibingu na mshambuliaji, Benson January waliotoka Biashara United.

Mapigano anakumbukumbu nzuri katika Ligi ya Championship ambapo anashikilia rekodi ya kipa pekee aliyefunga bao akiwa na timu hiyo ya Biashara United msimu uliopita, wakati iliposhinda mabao 2-0, dhidi ya Polisi Tanzania, Februari 15, 2024.