Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa Yanga, Dodoma Jiji yawekewa Sh30 milioni mezani

UONGOZI wa Dodoma Jiji umeendelea kuweka mkazo kwenye mechi zao baada ya kutangaza dau la Sh30 milioni iwapo watatoka na ushindi kwenye mchezo wao wa Ligi dhidi ya Yanga.

Dodoma Jiji na Yanga zitakutana kesho Jumanne Novemba 22 mchezo utakaochezwa saa 10:00 jioni katika uwanja wa Liti, Singida.

Inaelezwa mabosi wa Dodoma Jiji wameweka dau hilo ili kuwapa motisha wachezaji wao kuhakikisha wanatoka na ushindi kwenye mchezo huo.

Mmoja wa watu wa karibu na viongozi wa juu katika timu hiyo anasema; "Wachezaji wamewekewa milioni 30 na watapewa endapo watashinda mchezo huo."

Uongozi wa Dodoma Jiji umekuwa na kawaida ya kuweka bonasi kubwa kwa wachezaji wao kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri hasa kwa timu kubwa.

Dodoma Jiji inashika nafasi ya pili kutoka mwisho (15) ikiwa na pointi tisa kwenye mechi ilizocheza huku Yanga ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 26 kwenye mechi 10 ilizocheza.