Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kinda la Yanga laingia kikosi bora

Kinda Pict

Muktasari:

  • Mtita pamoja na Isaack Emmanuel ‘Mtengwa’ wapo Wakiso kwa mkopo wakitokea Yanga ya vijana U-20 ambako walifanya vizuri wakicheza baadhi ya mashindano, Mapinduzi Cup na Kombe la FA.

KINDA wa Yanga, Shaibu Mtita anayekipiga Wakiso Giants ya Uganda ameingia kwenye kikosi bora cha raundi ya 15 baada ya kufanya vizuri kwenye nusu ya msimu wa ligi ya nchi hiyo.

Mtita pamoja na Isaack Emmanuel ‘Mtengwa’ wapo Wakiso kwa mkopo wakitokea Yanga ya vijana U-20 ambako walifanya vizuri wakicheza baadhi ya mashindano, Mapinduzi Cup na Kombe la FA.

Kwa mujibu wa TUF UG orodha ya wachezaji 11 waliofanya vizuri mzunguko wa kwanza wa Ligi yumo Mtita kwenye eneo la beki wa kati.

Akiwa mchezaji pekee wa Wakiso aliyeingia kwenye orodha hiyo anadhihirisha uwezo mkubwa aliojaaliwa kwenye miguu yake na kichwani.

Timu hiyo imeonja ushindi mara mbili kati ya mechi 15, sare sita na kupoteza michezo saba ikikusanya pointi 12 huku ikisalia nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi.

Kwenye michezo 15, Mtita amecheza 13 kwa dakika 941.