Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kenya yalia na idadi ya mashabiki CHAN 

KENYA Pict

Muktasari:

  • Katika taarifa yake, Waziri wa Michezo, Salim Mvurya, alieleza kuridhishwa na utendaji wa mashabiki katika mechi ya mwisho ya makundi dhidi ya Zambia na hakukuwa na matukio yoyote ya usalama yaliyothiri michuano hiyo.

SERIKALI ya Kenya imewasilisha ombi rasmi kwa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) likitaka idadi ya mashabiki watakaoshuhudia leo, Ijumaa mechi ya robo fainali ya michuano ya CHAN 2024 kati ya Harambee Stars na Madagascar kuongeza hadi 48,000 kutoka 27,000 iliyoruhusiwa kutokana na vikwazo vya usalama.

Katika taarifa yake, Waziri wa Michezo, Salim Mvurya, alieleza kuridhishwa na utendaji wa mashabiki katika mechi ya mwisho ya makundi dhidi ya Zambia na hakukuwa na matukio yoyote ya usalama yaliyothiri michuano hiyo.

Alisisitiza serikali imejizatiti kuhakikisha mazingira salama kwa mashabiki na wachezaji. “Hatukuona tukio lolote linaloweza kuathiri mashindano haya na tunashukuru mashabiki kwa ushirikiano wao,” alisema Mvurya.

Aidha, Mvurya aliongeza, Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) limewasiliana na CAF ili kujadili ongezeko la idadi ya mashabiki na wanatarajia majibu katika muda mfupi.

Kwa upande mwingine, ili kupanua wigo wa mashabiki, FKF imeongeza maeneo rasmi ya mashabiki kushuhudia mechi hiyo (fan zones) kutoka 10 hadi 13 katika Jiji kuu la Nairobi, ikiwa ni pamoja na maeneo mapya ya Ruiru, Camp Toyoyo (Dagoreti), na Babadogo.

Vilevile, maeneo sita mapya yameanzishwa Mombasa, ikiwa ni pamoja na Uwanja wa Volleyball wa Changamwe, Uwanja wa St. Mary’s Bangladesh (Jomvu), Uwanja wa Mama Ngina Waterfront (Mvita), Uwanja wa Shelly Beach (Likoni), Uwanja wa Hassan Joho (Nyali) na Uwanja wa Bilima (Kisauni).