Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Karia atoa tuzo tatu za heshima

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia ametoa tuzo tatu kwa watu waliochangia mafanikio ya soka nchini huku tuzo ya kwanza ya heshima ikienda kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Tuzo ya Mama Samia imetolewa kwa kutambua mchango wake mkubwa anaoufanya kwenye michezo ambapo Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma ndiye aliyepokea kwa niaba.

Tuzo ya pili ya Heshima ilienda kwa marehemu Angela Bilali aliyetoa mchango mkubwa kwenye soka la wanawake wakati tuzo nyingine ya mchezaji gwiji wa zamani iliyokwenda Leopard Tasso Mkebezi ambaye kwasasa ni kocha wa Chama cha Makocha Tanzania.

Tasso amepewa nafasi ya kuzungumza na kusema kuwa; "Nimecheza timu ya Taifa miaka miwili mfululizo bila kukaa benchi na kuwa meneja wa Stars wakati timu hiyo ipo chini ya Mbrazil Marcio Maximo."