Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kanali Bakari atunukiwa nishani ya michezo Russia

Kanali Bakari atunukiwa nishani ya michezo Russia

Wizara ya Ulinzi ya Jeshi la Shirikisho Urusi limemtunuku  nishani kwa kuimarisha ushirikiano katika Majeshi Kimataifa Kanali Joseph Bakari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania nchini Urusi.

Kanali Bakari ambaye ni Mkurugenzi wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani ( CISM ) alitunukiwa nishani hiyo kutokana na mchango wake na juhudi zake katika kusimamia maandalizi ya Michezo ikiwemo ya Maofisa wanafunzi yaliyoafanyika nchini humo hivi karibuni.

Mashindano hayo yaliandaliwa  kutokana na mgogoro unaoendelea kati ya nchi ya Urusi na Ukraine, na  yalikabiliwa na  changamoto kwa baadhi ya Wanachama  walitaka michezo hiyo isifanyike kwa nyakati tofauti kuanzia mwaka 2019 hadi 2022.

Nishani hiyo alivishwa na Naibu Waziri wa Ulinzi wa Jeshi la Shirikisho la Urusi Jenerali Nikolay  Pankov mbele ya viongozi mbalimbali wa Jeshi la Shirikisho la Urusi pamoja na wageni wengine wakiwemo washiriki kutoka nchi 20.

Kwa mujibu wa tovuti ya Wizara ya Ulinzi ya Shirikisho la Urusi, Nishani hiyo hutunukiwa kwa Wanajeshi wa Jeshi la Shirikisho la Urusi au Raia kutokana na mafanikio yao katika kuunda na kutekeleza sera ya nchi katika eneo la mahusiano na mashirikiano ya Kijeshi Kimataifa (international military cooperation).

Aidha nishani hiyo pia hutunukiwa wananchi wa Shirikisho la Urusi na mashirikisho ya Kimataifa na raia wa nchi nyingine ambao wamechangia kutekeleza kwa mafanikio jukumu maalum la Jeshi la Shirikisho la Urusi Kimataifa.

Pamoja na Kanali Bakari wengine waliotunukiwa  Nishani ni Meja Jenerali Maikano Abdullahi kutoka Nigeria ambaye ni Rais wa Baraza la Michezo ya Majeshi barani Afrika na Mitryshin Alexei kutoka Urusi ambaye ni Rais wa Shirikisho la mchezo wa Rugby nchini Russia.